Mabondia Omary Ramadhani kushoto na Deo Njiku wakitunishiana misuri baada ya kusaini mkataba kupigania ubingwa wa Tanzania PST siku ya February 14 katika ukumbi wa Friends Corner Hotel Manzese picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Na Mwandishi Wetu
MABONDIA Deo Njiku wa Morogoro na Omary Ramadhani wataingia uringoni February 14 katika ukumbi wa Friends Corner Hotel Manzese 14 kuwania Ubingwa wa Tanzania PST
Mpambano huo wa aina yake unatarajiwa kuwa wa kusisimua kutokana kila mtu kuwa na rekodi nzuri mpambano uho utakaosindikizwa na mpambano mwingine wa ubingwa kati ya Godfrey Silver na Adam Yahya ambapo mipambano hiyo itakuwa ya raundi kumi.
Huku kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi Nchini, Rajabu Mhamila 'Super D' atampandisha kwa mara ya kwanza bondia wake mpya Iddy Mnyeke kuvaana na Sadiki Momba mpambano utakaopigwa kwa raundi nne
Mgeni rasmi siku hiyo anatsrahjiwa kuwa ni Kamanda wa polisi mkoa wa Kipolisi wa kinondoni Charles Kenyela atakaewafisha mikanda ya ubingwa
Super D, alisema katika mpambano huo atasambaza DVD zake mpya tofauti na kanda yake ya awali iliyokwenda kwa SUPER D BOXING COACH, DVD za sasa zimeandaliwa kisasa na zikiwa na mchanganyiko wa ‘clips’ za michezo ya nyota wa Dunia katika kuwafunza watu namna ya kupigana ngumi.
Aliongeza kuwa, mbali na dvd hizo bado wanaitajika vijana wenye vipaji kujitokeza kuja kushiriki katika mazoezi ya ngumi ili wajiunge na wenzao wa
timu ya Ashanti na Amana kujifunza ‘live’ chini ya makocha Habibu Kinyogoli, Kondo Nassoro, na yeye mwenyewe Super D na wengine wanaowanoa vijana