Na Hellen Kwavava wa Kajunason Blog, Dar es Salaam.
Uongozi wa Jumuiya wa wanafunzi wa elimu ya Juu nchini (TAHLISO) umesema kwamba wamejipanga kufanya maandamano ya amani ifikapo tarehe 25 ya mwezi huu kama serikali haita timiza ahadi waliyoitoa kwa kuwalipa kiasi cha shilling billion 6.6 zilivyobaki kama hela ya mafunzo kwa vitendo ifikapo wiki ijayo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Musa Mdede ameeleza kwamba lengo la kubwa ni kuitafuta haki yao ya msingi ambapo wao kama uongozi unapata wakati mgumu kuona kwamba wanafunzi wenzao hawajapata fedha za mafunzo kwa hasa ukizingatia siku walizopewa kufanya mafunzo hayo zimekaribia kwisha.
Naye Rais wanafunzi katika Chuo cha Sauti Mwanza Simon Phillibert amesema kwamba anashindwa kukaa na kuendelea na majukumu mengine kama kiongozi ya kimasomo ikiwa bado hawana jibu kamili kwanini hadi wakati huu hawajapata mkopo na bado serikali ipo kimya bila kutoa tamko lolote lile.
Wakati huo huo Rais wa Chuo cha DIT, Dar es Salaam Emili Heri huruma “amesema kwamba inashangaza waziri mwenye dhamana katika sekta ya elimu bado yupo kimya kuhusiana na suala hili”
Usiku wa siku ya Alhamisi wiki hii Uongozi huo wa Tahliso ulikamatwa na polisi kwa madai kuwa wamejipanga kufanya maandamano ya uchochezi kinyume na sheria ambapo siki ya Ijumaa Uongozi wa polisi kupitia kanda kinondoni waliwaachia kwa dhamana.