Na Hellen Kwavava wa Kajunason Blog, Dar es Salaam.
Makamu wa rais nchini dakta Gharib Bilal anatarajia kufungua kongamano la tatu la Sayansi ya Dunia litakalo wahusishwa vijana wanaosomea taaluma hiyo lengo kuu likiwa kurithisha ujuzi huo kizazi hadi kizazi.
Akizugumza na waandishi wahabari mtedaji mkuu wa taasisi ya wakala wa Geologia nchini professa Abdlukarim Mruma amesema kwamba wamefanya hivyo kwa kuwa taaluma hiyo ya sayansi ya dunia imeenea katika sekta nyingi duniani.
Naye mwalimu wa chuo kikuu cha Dodoma Michael Msabi ameeleze kuwa kongamano hilo lizungumzia vitu vingi vinavyo igusa dunia ambapo tafiti mbalimbali zilizofanywa na vijana hao zitakuwepo ili kuweza kutoa mwaga kwa watu kuhusiana na elimu hiyo ya Geologia.
Kongamano hilo nila siku nne lina lengo la kuwakutanisha vijana chini ya miaka 35 ambapo likimalizika litakuja kongamano lingine la pili litakalo husu masuala ya geologia ya afrika na manufaa yanayotokana na taaluma hiyo.