Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

TTCL YAJA NA HUDUMA MPYA YA BWERERE

$
0
0
 Afisa Mkuu wa Masoko na Mauzo TTCL, Peter Ngota akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano wa uzinduzi wa huduma hiyo katika makao makuu ya kampuni ya TTCL mtaa wa Samora jijini Dar es salaam. 
  Wafanyakazi wa TTCL nao hawakuwa nyuma kufuatilia uzinduzi huo.
 Baadhi ya wanahabari wakiwajibika kwenye mkutano huo.
---
Natumia fursa hii kuwakaribisha wanahabari, wageni waalikwa na wafanyakazi wenzangu wa TTCL katika ukumbi huu ambapo leo tuna tukio muhimu la uzinduzi wa huduma mpya inayo waleta watu karibu zaidi. Ninayo furaha kubwa katika siku hii ya pekee kuujulisha umma kuwa TTCL inatoa fursa kwa wateja wake na umma kwa ujumla kutumia mtandao wa TTCL kupata huduma ya mawasiliano BORA ya simu na intaneti kwa bei nafuu zaidi.

Siku ya leo ,TTCL inazindua rasmi promotion inayolenga kuwapa wananchi huduma bora na za bei nafuu. Promotion hii inajulikana kwa jina la BWERERE yaani pata huduma nyingi zaidi kwa bei nafuu zaidi.

Promosheni hii inatoa fursa kwa wateja wa majumbTani na maofisini ambao wanatumia huduma ya malipo ya kabla(pre-paid) kufurahia gharama ya viwango vya chini kabisa vya kupiga simu TTCL kwenda kwenda mitandao mingine yote ikiwa ni pamoja na TTCL yenyewe.

Vilevile Promosheni hii inatoa fursa maalumu kwa watumiaji wa vifurushi vya intaneti(DATA) kwa njia ya Broadband mtandao wa Nyaya na Mkongo waTTCL kitaalamu Fixed lines kuweza kupata intaneti bila kikomo.

Ndugu wanahabari, Wageni waalikwa

Mbali na hayo Promosheni hii ya BWERERE inatoa fursa kwa mteja kupata huduma mbalimbali; Muda wa maongezi wa BURE na Data kwa wakati mmoja na kwa bei nafuu sana.
Huduma hizo ni kama zifuatazo;

• Tsh 1 kwa sekunde:- Mteja atapata fursa ya kupiga simu kwenda mitandao mingine kwa shilingi 1 kwa sekunde. Huduma hii haina kujiunga. Kabla ya hapo, kupiga simu TTCL kwenda mitandao mingine ilikuwa ikigharimu Tsh 230 kwa dakika 1. Kwa sasa mteja wa TTCL ataweza kupiga simu katika mitandao mingine na kuweza kuongea na ndugu, jamaa na marafiki kwa Tsh 1 moja kwa sekunde yaani kwa gharama ya shilingi sitini kwa dakika 1; Sawa na punguzo la Asilimia zaidi ya 70%

• Bwerere Premium:- inahusisha wateja wanaotumia huduma ya intaneti kuanzia kiwango cha 2Mbps mpaka 32 GB watapata fursa kupiga simu TTCL kwenda TTCL bure ndani ya mwezi, pia mteja atapata muda wa maongezi kuanzia dakika 300 mpaka dakika 600 kupiga simu kwenda mitandao mingine ndani ya mwezi.

• Bwerere Unlimited:- huduma hii inahusisha watumiaji wa intaneti kuanzia kiwango cha 512Kbps mpaka 2Mbps watapata huduma ya muda wa kupiga simu bure TTCL kwenda TTCL kwa muda wa mwezi mzima.

• Bwerere:- kwa watumiaji wa intaneti njia ya Broadband kuanzia 3 GB mpaka 24 GB watapata fursa ya kupiga simu bure TTCL kwenda TTCL.

Tunaendelea Kupanua Wigo wa uchaguzi wa huduma za vifurushi kwa watumiaji na kuwapa fursa ya waTanzania kutumia huduma za TEHAMA kwa bei nafuu kwa maendeleo ya M-Tanzainia na Taifa.

TTCL inapenda kuutarifu umma faida za simu za mezani, Simu za mezani katika mawasiliano na maendeleo kwa ujumla kama ifuatavyo;

1. Simu za mezani zinausalama mkubwa sio rahisi kwa mtu kuingilia mawasiliano ambayo yanatolewa kwa njia ya waya yaani kitaalamu cable.

2. Vilevile simu za mezani ni nzuri sana kwa matumizi ya kiofisi na majumbani, ni rahisi kutambua sehemu ya ofisi au nyumba unayoishi, pia Ni simu ambazo zinakuthibitishia uwepo wa mtu unayewasiliana naye katika eneo husika.

3. Mwisho, simu za mezani mawasiliano yake yana ubora mkubwa na uhakika kiusikivu na kasi zaidi kwa intaneti.

Napenda kuitimisha kwa kuwakaribisha wateja wote, na ninyi wanahabari kufurahia huduma hii ya BWERERE ambayo inakupa huduma nyingi kwa wakati mmoja.

TTCL ni kampuni pekee hapa nchini ambayo inatoa huduma za DATA, simu zenye ubora zaidi. Ni mtandao pekee ambao umeenea katika mikoa na wilaya zote nchini.

Sasa ni wakati mzuri wa kutumia na huduma hii ya BWERERE na Ufaidike zaidi na TTCL kwa UBORA wa huduma na gharama nafuu zaidi nchi nzima.

TTCL HULETA WATU KARIBU.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

Trending Articles