Hatimaye uchaguzi wa nafasi ya Rais wa TUCTA umefanyika na kuzaliwa matunda ya Mukoba Gratian (56) ambaye amejinyakulia kiti hicho.
Akieleza katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii mmoja ya wagombea Bw. Dismas Lyassa alifafanua kuwa sababu za yeye kutoshinda... moja ni udhaifu wa chama nilichopitia yaani Cotwu ambacho kina wajumbe 18, wakati chama cha walimu cha Mukoba kina zaidi ya wajumbe 42 wanaopiga kura. WAJUMBE WANAPATIKANAJE? Kutokana na wingi wa wanachama..., ni kama ilivyo kwa vyama vya siasa kadri unavyokuwa na wabunge wengi ndivyo unavyokuwa na wabunge wengi wa viti maalum... Rushwa ni sababu nyingine wapo wajumbe nilipopita kuwapa vipeperushi waliniambia vipeperushi vyangu vyepesi..wakitaka rushwa...kitu ambacho siwezi kufanya. Nimejifunza mambo mengi yanayoweza kuibua safari nyingine... Endelea kufuatilia ataeleza mengi.