Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

TAMASHA LA KUTOA ELIMU YA ATHARI ZA DAWA ZA KULEVYA KUFANYIKA SEPTEMBA DAR

$
0
0
Na Winner Abraham-MAELEZO-Dar es salaam

Uongozi wa ZION SOUNDS umeandaa tamasha la kuelimisha jamii kuhusu athari za dawa ya kulevya linatarajia kufanyika mapema mwezi ujao.

Tamko hilo limetolewa na Mtendaji Mkuu wa ZION SOUNDS Bw. Junior Zion wakati wa mkutano na waaandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa wameamua kuandaa tamasha hilo ili liweze kuwaelimisha vijana kuacha kujiingiza katika utumiaji wa dawa za kulevya

“Kama tunavyojua kuwa vijana ndio viongozi wa baadaye hivyo wanahitaji msaada mkubwa katika makuzi na kuelimishwa ni jinsi gani wataepukana na janga hili hivyo wahamasishwe kwa njia tofauti tofauti”amesema Zion

Ameongeza kuwa kwa takwimu za nyuma kidogo karibu ya asilimia 40% ya vijana tayari wanatumia dawa za kulevya kama Cocaine na bangi.

Naye Meneja Matukio wa Zion Sounds Bi.Careen Dora Bi Careen ametaja sababu zinazochangia vijana wengi kujiingiza katika matumizi ya dawa na pombe kuwa ni kama kutaka kujua kwani kipindi cha ujana ni kipindi ambacho wengi hutaka kujua vitu vingi ambavyo ni vigeni kwao.

Amesema kuwa vijana wanaoanza kutumia pombe wakiwa na umri wa miaka 15 wanaathirika mara 5 zaidi wanapofikia umri mkubwa.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>