Na Hellen Kwavava wa Kajunason Blog, Dar es Salaam.
Zaidi ya dollar billion 121.6 kwa mwaka zimeweza kuokolewa nchini katika uingizaji wa mafuta baada ya kuanza kutumia mfumo wa uingizaji wa mafuta kwa pamoja ambao umeanza januari mwaka 2012.
Mfumo huo umeweza kuokoa muda wa kuweza kupakua mafuta bandarini kutoka siku 60 hadi tatu na pia udhibitiwa ubora wa mafuta umeongezeka kwa kiasi kikubwa.
Hayo amebainisha Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka ya udhibitiwa Nishati na maji (EWURA) Felix Ngamlagosi wakati akifungua mkutano wa wadau toka taasisi mbalimbali nchini na nje ya nchi kwa lengo la kujadili na kutoa maoni yao kuhusiana na mfumo huo ili kuweza kupunguza gharama katika uchumi na kwa mtumiaji.
Felix amesema kwamba mfumo huu una uhakika zaidi kwa kutoa takwimu sahihi katika mafuta yote yanayotumika kwa ajili ya matumizi nchini.
Naye mdau kutoka benki ya NMB bi Wende Mengele ameeleza kwamba kutokana na mfumo huu kutaweza kuleta faida kwa wananchi pamoja na kwa benki kutakuwa na mfumo mzuri unaoeleweka.
Hatahivyo EWURA bado wanaendelea kupokea maoni kutoka kwa wadau mbalimbali wa uchumi hadi ifikapo Agosti 4, 2014 mwaka huu na baada ya hapo kuanza kuyafanyia kazi kwa kuyaweka pamoja huku wakishirikiana na benki kuu.