Moja ya kichwa cha binadamu kilichotolewa kwenye mifuko hiyo.
Miguu iliyokaushwa ikiwa kwenye mifuko. Picha kwa hisani ya Daresalaam-yetu.blogspot
Gari likiwa limebeba mifuko yenye viuongo hivyo, ambapo Jeshi la Polisi wilaya ya Kinondoni limesema kuwa limeanza uchunguzi wa kina baada ya kukakamata viungo mbalimbali vinavyodhaniwa kuwa ni vya binadamu katika mifuko ya plastiki katika machimbo ya kokoto sehemu za Mbweni Mpiji, Magohe, nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.
HABARI ZA AWALI TOKA KWA MASHUHUDA WA TUKIO:Habari zilizotufikia usiku wa leo Julai 21, 2014 maeneo ya Bunju B jijini Dar es Salaam watu wawili ambao walikuwa na gari dogo aina ya Isuzu wamekamatwa na Jeshi la Polisi wakiwa viungo vya binadamu ambayo walikuwa wameifunga katika mifuko ya plastiki.
Taarifa zilizotufikia zinasema kuwa dereva wa gari hilo alifanikiwa kumwaga viungo safari ya kwanza (Trip) eneo la shule ya Consolata ya Masista na aliporudi kumwaga awamu ya pili ndipo wananchi walipowaita polisi na kufanikiwa kumkamata dereva huyo.
Polisi wa Kituo cha Bunju A na Wazo waliamua kupiga risasi hewani ili kuweza kuwatawanya watu waliovamia Kituo cha Polisi Bunju A wakiwa na lengo la kumuua dereva aliyekamatwa akiendesha gari hilo lililokuwa limejaa viungo hivyo.
Endelea kufuatilia sakata hilo.