Picha juu na chini ni tukio lililotokea leo majira ya mchana barabara ya Mwai Kibaki maeneo ya TMJ Hospital jijini Dar es Salaama ambapo majambazi yalikuwa yakikimbia kwa mguu yakitokea Msasani kwa Mwalimu Nyerere walilishambulia basi la wafungwa la Magereza lililokuwa likisindikizwa na gari lingine nyuma lililokuwa na askari Magereza. Shambulio hilo limewajeruhi wafungwa na baadhi ya askari hao wa Magereza, hakuna mtu aliyekufa na majambazi yametokomea kusikojulikana.
↧