Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

ENZI HIZO: SHERIA 13 ZA MPIRA WA MIGUU WAKATI TUKIWA WATOTO

$
0
0
1. Mtoto mnene lazima awe Golikipa

2. Mtoto aliyekuja na mpira ataamua nani acheze na nani asicheze.

3. Penati itatokea tu pale mchezaji akiumia sana na kutoka damu.

4. Mechi itaisha kama kila mchezaji atakua amechoka.

5. Hakuna free kick, kitu kama hicho hakipo kwenye mechi zetu.

6. Hakuna Refa, mchezaji anaweza kuzunguka na mpira ata nyuma ya goli.

7. Kama haushiriki kwenye kutengeneza mpira unaweza usipate namba uwanjani.

8. Ukichaguliwa mwishoni ujue uwezo wako ni mdogo kuliko watu wote uwanjani.

9. Wale ambao wamekosa namba kazi yao ni kufata mpira ukitoka, au kutungua mpira endapo utanasa kwenye mti huku wakisubiria mchezaji aitwe kwao na wao wapate nafasi.

10. Mwenye mpira akikasirika, mechi ndio itakua imefika mwisho.

11. Inaruhusiwa kubadili golikipa kama penati ikitokea na baada ya penati golikipa anaweza kuendelea na alipokuwa anacheza mwanzo.

12. Yule mtaalam wa soka huwa hakosi namba ata siku moja.

13. Mwenye mpira huwa hatolewi ata akicheza vibaya.

Imeandaliwa na Joseph Stima Ulaya.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>