Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU KUWASHTAKI WAAJIRI WAZEMBE

$
0
0


Mkurugenzi Msaidizi Urejeshaji Mikopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Bw. Robert Kibona akitoa mada wakati wa mkutano mkuu wa mwaka wa Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Serikalini mjini Dodoma leo.
Baadhi ya washiriki wa mkutano mkuu wa mwaka wa Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Serikalini wakifatilia mada mjini Dodoma leo.
---
Na Mwandishi Wetu, Dodoma.


Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu nchini imepanga kuwachukulia hatua waajiri wote nchini kwa kushindwa kuwasilisha taarifa za wahitimu wa elimu ya juu wanaodaiwa na Bodi hiyo.

Hayo yalisemwa na Mkurugenzi Msaidizi Urejeshaji Mikopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Bw. Robert Kibona alipokuwa akitoa mada kuhusu urejeshwaji wa mikopo ya elimu ya juu kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu Serikalini mjini Dodoma leo.

“Mpaka sasa tumewachukulia hatua jumla ya waajiri watano ambao wameshindwa kuwasilisha taarifa za watumishi wao wanaodaiwa na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu” alisema Bw. Robert.

Alisema, mwajiri atakayeshindwa kutoa taarifa za wahitimu wa elimu ya juu katika Bodi kwa wakati atatakiwa kulipa faini ya shilingi milioni saba au kutumikia kifungo kisichopungua miezi 12 au vyote kwa pamoja.

Aidha, Bw. Robert alisema kuwa mpaka sasa takribani waajiriwa 18 wamefikishwa mahakamani kwa kosa la kushindwa kurejesha mikopo hiyo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>