Na Mwandishi Wetu, Dar es salaam
BAADA ya mizengwe kugubika uchaguzi wa Simba sc , sasa kimeeleweka baada ya mahakamu kuu kuruhusu mchakato huo kuendelea kama kawaida.
Baadhi ya wanachama wa Simba walienda mahakama kuu wakihitaji chombo hicho cha dola kusimamisha uchaguzi wa Simba unaotarajia kufanyika juni 29 mwaka huu.
Sababu ya wanachama hao ilikuwa ni kupinga maamuzi ya kamati ya uchaguzi ya Simba, chini ya mwenyekiti wake, Wakili Damas Daniel Ndumbaro, kuliengua jina la aliyekuwa mgombe wa Urais, Michael Wambura kwa mara ya pili.
Hii hapa ni kauli ya katibu mkuu wa Simba, Ezekiel Kamwaga aliyotoa jioni hii.
“Uchaguzi upo Jumapili, Mahakama imeruhusu. Kazi kwenu wana SIMBA”.
Hata hivyo, suala la wanachama kupelekea suala la michezo katika mahakama ya kawaida ilikuwa ni hatari zaidi kwa klabu ya Simba kwasababu sheria za mpira ziko wazi na hairuhusiwi kupeleka mambo ya mpira mahakama za dola.
Simba SC inapenda kuwaalika wanachama wote katika Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Klabu uliopangwa kufanyika Keshokutwa Jumapili, Juni 29 mwaka huu, katika Ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi, Oysterbay jijini Dar es Salaam.