Marehemu Tyson akikata cake yake ya harusi pamoja na mke wake Monalisa
Baada ya maneno maneno mengi kuhusu Monalisa na marehemu George Tyson mwandada huyo ambae alikuwa mke wa Tyson amefunguka kwa kuandika ujumbe ufuato kupitia ukurasa wake wa Instagram, na nukuu:
"Let me clear the air. ni hivi, pamoja na ujinga tulioufanya mimi na George katika maisha yetu, kwa macho ya kibinadamu utasema alikuwa na mke mwengine... but kwa macho ya kiMungu mimi ni mke halali wa George Otieno Okumu aliyelala. anayesema mke wa Tyson alijifungia ndani mimi nikawa nachukua pole zisizo zangu, dah! kwanza wanawake walikuwa wawili ndani sio mmoja na wote walijifungia ndani, kwanini? ni wakristo na wanaijua dini. Waombolezaji waliokuwa wakinipa pole mimi, ni kwanini? jiulize kabla ya kuropoka halafu wewe ni mwanamke kuna siku yatakukuta.
Nilienda Nairobi, Kenya kutimiza wajibu wangu kama mke, ningelia peke yangu kwetu mngenisema sana, nimekaa msibani naambiwa nachukuwa pole za bure. Wacha nikukumbushe maandiko... Alichokiunganisha Mungu?....; kilichofungwa duniani?.....; nikupende, nikutunze hadi kifo?..... sasa kifo kimetutenganisha. Siku ya mwisho unadhani George ataitwa na nani? pamoja na mambo yake yote wacheni nimlilie he was a good father kwa Sonia wangu esp. miaka 5 ya mwisho wa uhai wake acheni nimlilie he was my best friend 1998-2014. Nimeshare nae kitanda 2000-2006 nitakuwa mtu wa aina gani nisiwe na uchungu? ukiona mwanamke mwenzio kaishindwa ndoa usimcheke jua kuna sababu... na ni fundisho kwa wachukua waume za watu wote mjini, mume akiumwa huwa anarudi kwa mkewe, na akifa? and for your info... msianze anajifanya mke sasa hivi ili apewe mali... Sonia ni mali kubwa sana alioniachia am so happy. Waaache wao wanaolilia kupewa pole wapiganie. Mwenyewe aliyetafuta kafa kaziacha sembuse tuliobaki? niacheni nimlilie, waacheni fans wangu walie na mimi.
Yatosha... ila napenda kuwashauri tu hata siku moja usicomment kitu ambacho hukijui, ni mbaya sana. na mtu usikurupuke kucomment kabla hujasoma na kuelewa vizuri ila ndiyo watanzania tulivyo, watu wanakujua kuliko unavyojijua... na siku zote mwanamke akifanya kinaonekana kibaya kuliko mwanaume nyie mnaongea ongea tu laiti mngeujua ukweli, ee Mungu nipe subra ile post naifuta maana naona nawapa watu ela na kik za bure. Pole kwa wote waliokereka na pole kwa wote mnaoomboleza pamoja nasi. Pumzika kwa Amani Baba Sonia"