Jiji la Mwanza ni mji nchini Tanzania ambao ni makao makuu ya Mkoa wa Mwanza. Mji upo kando la ziwa Viktoria Nyanza Kulingana na sensa ya mwaka 2002 idadi ya wakazi wake ilihesabiwa kuwa 378,327 (ukijumlisha wakazi wa Wilaya ya Nyamagana na sehemu za Wilaya ya Ilemela).
Mwanza ilianzishwa na Wajerumani wakati wa koloni ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani. Mahali paliteuliwa kutokana na nafasi ya bandari asilia upande wa kusini ya Ziwa Viktoria. Wajerumani waliuita mji kwa jina "Muansa" inaaminiwa ilikuwa matamshi yao ya neno "nyanza". Walijenga boma kubwa iliyoendelea kitovu cha mji. Takwimu ya Kijerumani ya 1912 ilihesabu wazungu 85, Wagoa 15, Wahindi wengine 300 na Waarabu 70 lakini haikutaja wakazi Waafrika. Palikuwa na makampuni ya biashara 12 ya kizungu na 50 ya Wahindi.
Katikati ya jiji.
Barabara za katikati ya mji.