Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

AIRTEL YATOA MSAADA WA VIFAA VYA OFISI KWA SHULE YA MSINGI CHAU, CHALINZE

$
0
0
Airtel Afisa mauzo wa kanda ya Pwani William Mrocky akikabithi kwa mwalimu mkuu wa shule ya msingi Chau Bwana Elvin Msangi msaada wa viti na meza kwaajili ya ofisi ya walimu wa shule ya msingi ya chau iliyoko Chalinze Mkoani Pwani.

Na Mwandshi Wetu, Dar es Salaam.

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kupitia shughuli zake za huduma kwa jamii imetoa msaada vifaa kwa ajili ya ofisi ya walimu kwa shule ya msingi ya Chau iliyoko Chalinze mkoani Pwani.

Akiongea kwa niaba ya Airtel Afisa mauzo wa kanda ya Pwani William Mrocky alisema” leo tunayofuraha kutoa msaada wa viti na meza kwaajili ya ofisi ya walimu shuleni hapa, msaada huu unalenga katika kuboresha mazingira ya ofisi na kuwawezesha walimu kufanya kazi zao kwa ufanisi zaidi.

Huu ni mwendelezo wetu wa huduma kwa jamii hususani katika sekta ya elimu ambapo kupitia mradi wetu wa “shule yetu” tumeziwezesha shule mbalimbali za sekondari kupata vitabu vya ada na kiada na kukabili changamoto za uhaba wa vitabu mashuleni. Sambamba na vitabu pia tunatoa msaada wa madawati na vifaa vya ofisi kama tunavyofanya leo katika shule hii ya msingi Chau

”Tunaamini msaada huu utaleta tija na kuboresha utendaji wa kazi kwa walimu shuleni hapa” aliongeza Mrocky

Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule ya msingi Chau bwana Elvin Msangi alisema” nashukuru sana Airtel kwa kutufikia shuleni hapa, hii ni mara yakwanza kupokea msada kama huu shuleni hapa hivyo tunajisikia faraja kuona kampuni kama ya Airtel inafanya kazi kubwa katika kusaidia sekta ya elimu. Tunayo mahitaji mengi hapa shuleni, Tunategemea huu ni mwanzo hivyo mtatumkumbuka katika program zetu itakayokuja siku za usoni.

Msaada huu utawawezesha walimu kuwa na ofisi nzuri na kuwaboreshea mazingira yao ya kazi kuwa bora zaidi.

Airtel kupitia mradi wake wa shule yetu unaziwezesha shule mbalimbali nchini kufaidia na vitabu, zaidi ya shule 900 nchini zimefaidika na mradi huu mpaka sasa.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>