Wa kwanza Kushoto ni Mkurugenzi mkuu wa Heineken Tanzania, Uche Unigwe akikabidhi zawadi kwa washindi wa mchezo wa Foosball, Ntoli Mwaikambo na Eric Duncan Lissa. Washindi hawa walikuwa wakiwakilisha bar ya Didi's, iliyopo Masaki jijini Dar es Salam.
Mkurugenzi mkuu wa Heineken Tanzania, Uche Unigwe (kwanza kushoto), akimkabidhi mfano wa hundi yenye dhamani ya dola za kimarekani $10,000 kwa mmiliki wa bar ya Didi’s, Bw. Hillary Marc Mremi mara baada ya vijana wake kuweza kufanikiwa kupata ushindi. Wanaoshuhudia ni Ntoli Mwaikambo, Eric Duncan Lissa.
Wachezaji wa timu ya Didis, Eric Duncan Lissa (wa kwanza kushoto) akiwa na mwenzake Ntoli Mwaikambo wakichuana vikali na Said Duche (wa kwanza kulia) na Abdala Kassim wa Hasadam , katika fainali ya soka ya mezani 'foosball' iliyofanyika jumamosi katika ukumbi wa Club 777 uliopo Kawe, Dar es salaam. Timu ya Didi’z iliibuka kidedea kwa magoli 9-3 na hivyo kushinda nafasi ya kwenda Ibiza Hispania kwa udhamini wa Heineken foosball.
Mkurugenzi mkuu wa Heineken Tanzania, Uche Unigwe akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani.)
Na Mwandishi Wetu
TIMU ya Didi’s ya mchezo wa mpira maalum wa meza ‘Foosball’, juzi walifanikiwa kutwaa ubingwa wa mashindano hayo nchii baada ya kuifunga timu ya Amsterdam kwa magoli 10-6.
Kwa ushindi hu timu hiyo yenye wachezaji wawili wamafanikiwa kupata nafasi ya kwenda Ibiza kuangalia fainali ya klabu bingwa Ulaya.
Mashindano hayo ya Foosball yaliyoanza mwezi uliopita yaliandaliwa na kudhaminiwa na Heiken ambao ndio wadhamini wa ligi ya mabingwa Ulaya.
Akizungumza wakati wa ufungaji wa mashindano hayo, Meneja wa Heiken Tanzania, Uche Unigwe, alisema kuwa mashindanp ya mwaka yamefanyika katika kiwango kikubwa na hamasa ya mchezo huo hapa nchini imekuwa kubwa.
“Kumalizika kwa msimu huu ni maandalizi kwa ajili ya msimu ujao, mwakani tumejipanga kuyaboresha zaidi kwa sababu tueona jinsi yanavyokuwa,” alisema Uche.
Kwa upande wao, washindi kutoka timu ya Didi’s, Ntoli Mwaikambo na Erick Duncan Lissa, walisema kuwa mashindano ya mwaka huu yalikuwa magumu lakini wamefurahi kutwaa ubingwa na kupata nafasi ya kwenda Ibiza.
Mashindano ya mwaka huu yalishirikisha zaidi ya timu 16 kutoka sehemu mbalimbali za Dar es Salaam ambapo yalizinduliwa rasmi Machi 18 na kumalizika juzi.
ENDELEA KUSOMA ZAIDI »