Kipa wa timu ya Yanga, Juma Kaseja akifanya mazoezi katika Uwanja wa Karume Dar es Salaam jana kukabiliana na timu ya Simba wanayotarajia kushuka dimbani leo Aprili 19, 2014.Wakati timu za watani wa Jadi Yanga na Simba, zinashuka dimbani kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo Aprili 19,2014 katika mchezo wa kufunga dimba la Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Yanga itashuka dimbani ikiwa na machungu na kumbuku ya kufungwa mabao 5-0 na droo ya 3-3 katika mchezo waliokuwa washinde wa Nani Mtani Jembe uliopigwa dimba hilo hilo la uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Simba nao watashuka dimbani wakiwa na mahesabu magumu zaidi ya kujihami kutokubali kufungwa mao mengi au kama yale walioyowafungwa watani wao ama kutokea kile kilichotokea katika mechi ya nani mtani Jembe kwa kuanza kufungwa na kisha kufanya kazi ya kusawazisha.
Japo mchezo wa kesho hautakuwa na mvuto kama ambavyo timu hizo zingekuwa zinagombea nani atwae ubingwa na nani awe mshindi wa pili, lakini bado mechi hiyo itakuwa ni ngumu na si kama ambavyo wengi wanaifikiria kuwa itakuwa ni rahisi na hasa kama unavyojuwa pindi wanapokutana watani wa jadi.