Waendesha bodaboda wakiongoza msafara wa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kuelekea kwenye mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Kashaulili mjini Mpanda leo asubuhi wakati wa kuhitimisha ziara ya siku 21ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kuata Ilani ya CCM katika mikoa ya Rukwa,Kigoma na Katavi. PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Kinana akiwa na Meneja Mahusiano ya Umma wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Muungano Saguya (kushoto) na Meneja wa NHC Katavi, Nehemia Msigwa alipokuwa akikagu ujenzi wa nyumba za bei nafuu 90 eneo la Ilembo, mjini Mpanda , mkoani Katavi.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrhaman Kinana akipanda juu ya tangi alipokwenda kukagua mradi wa maji wa Ikolongo, eneo la Kazima, mjini Mpanda, Katavi leo.
Mjumbe wa NEC-CCM kutoka Zanzibar, Balozi Ali Abeid Karume (aliyevaa kofia) akipanda juu ya tanki kukagua mradi wa maji wa Ikolongo, mjini Mpanda leo.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisaidia kutandaza mabomba katika mradi wa maji wa Ikolongo, eneo la Kazima, Kata ya Kawajense, Mpanda Mjini, wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM katika Mkoa mpya wa Katavi. Kinana amehitimisha leo ziara ya kikazi ya siku 21 katika mikoa ya Rukwa, Kigoma na Katavi.
Balozi Thobias Kazimzuri wa Shina namba 32 la CCM la Makanyagio mjini Mpanda, akielezea mbele ya Kinana matatizo mbalimbali yanayowakabili katika eneo hilo.
Katibu wa Itkadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akicheza na watoto wakati wa mkutano katika Shina la CCM namba 32, la Makanyagio, Mjini Mpanda la Balozi Thobias Kazimzuri lililotembelewa na Katibu Mkuu wa CCM,Abdulrahman Kinana leo.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara katika viwanja vya Kashaulili, mjini Mpanda leo, baada ya kuhitimisha ziara ya siku 21ya kikazi ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM katika mikoa ya Rukwa, Kigoma na Katavi.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara katika viwanja vya Kashaulili, mjini Mpanda leo, baada ya kuhitimisha ziara ya siku 21ya kikazi ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM katika mikoa ya Rukwa, Kigoma na Katavi.