Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Green Stars Industry inayomiliki eneo la FAN CITY Bw. Hasan Rizvi akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) mashine za michezo mbali mbali itakayotolewa kipindi cha sikukuu ya Pasaka wakati wa mkutano alioufanya leo Aprili 17, 2014 katika eneo la Fun City Kigamboni jijini Dar es Salaam. Pia aliongeza kuwa kwa sasa kampuni yake imeeongeza mitambo yenye uwezo wa kutengeneza mawimbi ya aina sita tofauti kwenye bwawa kubwa la kuogelea.
Mitambo ya kisasa iliyofungwa katika eneo la Fun City ambayo itawawezesha wananchi kupata burudani kabambe zenye ubora wa kimataifa kwani hakuna mahali popote Afrika Mashariki mitambo hiyo.
Mawimbi yanayotengenezwa kwa mitambo ya kisasa katika bwawa kubwa la kuogelea lililopo hapa Fun City,
Moja ya Bwawa la kuongelea.
Mkurugenzi Mtendaji wa Fan City, Bw. Hasan Rizvi akionyesha vigari vya mchezo.
Bembea za kutosha.
Bembea za watoto.
Mapokezi ya Fun City.
Eneo la Fun City linasehemu ya Ibada.
Sehemu ya huduma ya kwanza nayo inapatikana hapa.
Sehemu ya moja ya sehemu ya bembea za magari ikiongesha madhari nzuri za kiota cha burudani cha Fun City.
Vigari vya umeme vinavyopita ndani ya maji.
*YAFUNGA MITAMBO YA KISASA KWA AJILI YA MICHEZO YA KWENYE MAJI
Na Mwandishi Wetu, Dares salaam
Wakati Watanzania wakiwa kwenye maandalizi ya sikukuu ya Pasaka kampuni ya Green Stars Industry inayomiliki eneo la FAN CITY limeongeza mitambo yenye uwezo wa kutengeneza mawimbi ya aina sita tofauti kwenye bwawa kubwa la kuogelea.
Mtambo huo wa aina yake utaongeza hamasa kwa waogeleaji kuhisi kama wapo baharini.
Akizungumzia mtambo huo Mkurugenzi Mtendaji wa Fan City, Bw. Hasan Rizvi amesema, lengo la kuoberesha michezo hiyo ni kuwawezesha watanzania kufurahia michezo hiyo pamoja na familia zao wakati huu wa Pasaka.
Ameongeza kuwa mitambo ya kisasa iliyofungwa katika eneo lake itawawezesha wananchi kupata burudani kabambe yenye ubora wa kimataifa kwani hakuna mahali popote Afrika Mashariki mitambo hiyo inapatikana.
“Tumefunga mtambo huu ambao utakua ukitengeneza mawimbi ya aina sita tofauti kwenye bwawa kubwa la kuogelea lililopo hapa Fan City, lengo letu nikutoa burudani zaidi kwa watu wanaotembelea hapa”.Alisema Rizvi.
“Tumefanya uwekezaji wa mashine za kisasa za michezo mbalimbali kwenye eneo letu ili kutoa burudani nzuri na za kipekee kwa wananchi wanaotembelea eneo hili na hasa wakati huu wa Pasaka”. Alisisitiza Rizvi. Fan City iliyopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Fun City imekuwa ikitoa burudani safi ya michezo mbalimbali kwa familia na katika kipindi hiki cha Pasaka imeandaa michezo kama Sarakasi, Mazingaombwe na zawadi kemkem kwa watakaotembelea eneo hilo.