Kutokana na kukithiri kwa mfumo dume unaoambatana na ukandamizaji wa mwanamke na kusababisha ongezeko la watoto yatima na wajane katika jamii ya wafuagaji wa kimasai, wanawake wa jamii hiyo wanaoishi ndani ya eneo la mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro wameunda baraza la wanawake litakalosimamia masuala mbalimbali kwa mtoto wa kike husani elimu,afya,na haki ya mwanamke.
Wanawake hao wa jamii ya kimasai wanabainisha kuwa hamasa ndogo ya jamii ya kuwasomesha watotot wa kilke na kutopewa kipaumbele ,afya duni ya jamii hasa mama na motto endapo vitazingatiwa katika jamii hiyo vitasaidia kuondokana na changamoto hizo na hatimae kuongeza idadi ya wasomi hasa watoto wa kike ambao wataikomboa jamii hiyo kwa ujumla .
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa baraza hilo uliofanyika katika makao makuu ya mamlaka ya hifadhi ya ngorongoro ukienda sambamba na harambee ya kuchangia mfuko wa elimu kwa watoto wa kike makamu mwenyekiti wa baraza hilo bibi mereyo muresi anasema litakua chombo muhimu cha kuwasemea wanawake katika vyombo vya maamuzi ndani na nje.
Mhifadhi mkuu wa mamlaka ya ngorongoro dakta fredy manongi ndiye aliyezindua baraza hilo na kuendesha harambee iliyofanikisha kupatikana kwa zaidi ya shilingi milioni sabini fedha taslimu na
ahadi.
Baraza la wanawake hao wafugaji linaanzishwa huku tayari kukiwa na baraza la wafugaji ngorongoro ambalo mwenyekiti wa baraza hilo metui ole
shaudo anawaasa kuwa lengo walilokusudia la kumkomboa mwanamke
litafikiwa kwa wao kushirikiana na wadau
wengine