Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

PICHA YA RAIS OBAMA YAZUA KIZAA ZAA

$
0
0
IKULU ya Marekani ‘White House’ imekilalamikia kitendo cha kampuni ya simu ya Samsung cha kutumia picha ya Rais Barack Obama aliyojipiga na mchezaji maarufu nchini Marekani, David Ortiz kama tangazo la kibiashara.

Picha hiyo ilipigwa na Ortiz mwenyewe akiwa na Rais Obama akitumia simu yake ya Samsung mapema wiki hii. Hata hivyo kampuni ya Samsung iliisambaza kupitia mtandao wa kijami wa Twitter kwa wateja wake na watu milioni 5.2 wanaoifuata kwa Twitter.

Msemaji wa White House, Jay Carney, alisema kuwa picha ya Rais haipaswi kwa njia yoyote kutumiwa kwa sababu za kujinufaisha kibiashara. Wakuu wa Samsung hawajasema lolote kuhusu malalamiko ya White House.

Ortiz mwenyewe alisema kuwa watu zaidi ya 40,000 waliisambaza picha hiyo kupitia Twitter
Bwana Carney alisema kuwa mawakili wa White House wanashauriana cha kufanya kuhusiana na kitendo hicho cha Samsung.

“Bila ya kusema mambo mengi, nataka niwaambie tu kwamba White House inapinga vikali jambo hili,” alisema Carney. Ortiz alimpa Rais Obama Jezzi maalum kutoka kwa klabu anayochezea ya Red Sox ikiwa na jina la Rais siku ya Jumanne na kisha kumshawishi kujipiga naye picha mwenyewe inayojulikana kama ‘Selfie’.

“Nilimpa Jezzi na wapiga picha wakatupiga picha, basi nilijihisi na mimi kujipiga naye picha” alisema mchezaji huyo. Hata hivyo alikana vikali ya kuwa kampuni ya Samsung ilimlipa pesa ili itumie picha hiyo.
-BBC

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>