Mkuu wa wilaya ya Rombo (kulia) akimkabidhi mwanafunzi Happnes John wa shule ya sekondari motamburu moja ya vitabu vya sayansi vilivyo tolewa na Airtell katika mpango wa shule yetu kwa shule ya sekondari Motamburu iliyopo Rombo mkoani Kilimanjaro.
Mkuu wa wilaya ya Rombo kulia akimkabidhi mwalimu mkuu (Abel Masuki kushoto) wa shule ya sekondari motamburu baadhi ya vitabu vya sayansi vilivyo tolewa na Airtell katika mpango wa shule yetu shuleni hapo
---
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania kupitia Program yake ya shule yetu imeendelea na zoezi lake la kuinua kiwango cha ufaulu katika masomo ya sayansi ambapo imekabidhi vitabu vya ziada na kiada katika masomo ya sayansi kwa shule ya sekondari ya MOTAMBURU iliyopo Kata ya tarakea wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro.
Akizungumzia msaada huo Meneja biashara wa Airtel kanda ya kaskazini Brightone Majwala alisema" program ya shule yetu inayolenga kutoa vifaa vya kufundishia mashuleni ikiwemo vitabu vya kiada na ziada kwa upande wa masomo ya sayansi ambapo mpaka sasa wameweza kufikia shule 900 katika baadhi ya mikoa ya Tanzania bara na visiwani ".
"Tutaendelea kushirikiana na serikali chini ya wizara ya elimu katika kuhakikisha tunaboresha elimu mashuleni na kupunguza changamoto za upatikanaji wa vitabu katika shule nyingi nchini. sliongeza Majwala