Mkuu wa Wilaya wa Songea Mjini, Joseph Mkirikiti akikata utepe kuashiria ufunguzi wa duka jipya la Tigo lililopo mjini Songea mtaa wa Shafi Bora asubuhi ya leo mkoani Ruvuma. Wakishuhudia kutoka kushoto ni Meneja wa Mauzo wa Tigo wa mkoa wa Ruvuma Kelvin Mibazi na Meneja wa duka hilo kutoka Tigo Wilfred Nestory.
Mkuu wa Wilaya wa Songea Mjini, Joseph Mkirikiti (kulia) akifurahia zawadi ya kadi ya kipaumbele aliyozawadiwa mapema leo na Mtaalam wa Huduma kwa Wateja kutoka Tigo Jackson Jerry. Kadi hiyo inampatia mteja wa Tigo huduma za kipekee kama kutokukaa katika foleni anapofika katika duka la Tigo pamoja na kuondelewa kwa gharama mbali mbali anapohudumiwa katika maduka hayo.
Mkuu wa Wilaya wa Songea Mjini, Joseph Mkirikiti akizungumza na wakazi na wateja wa Tigo kutoka Songea mjini (hawapo pichani) mapema leo. Mkuu huyo wa Wilaya aliipongeza Tigo kwa hatua hiyo ya kusogeza karibu huduma zake pamoja na kutoa ajira kwa vijana wa mkoani Ruvuma kupitia duka hilo.
Baadhi ya wateja waliohudhuria hafla fupi ya uzinduzi wa duka hilo la Tigo linalopatikana mtaa wa Shafi Bora Songea mjini wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya Joseph Mkirikiti alipofika kuzindua duka hilo mapema leo.
Mkuu wa Wilaya ya Songea Mjini Joseph Mkirikiti (mwenye suti) katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kampuni ya simu Tigo wa mjini Songea mapema leo.
---
Tigo leo imefungua duka jipya la huduma kwa wateja mjini Songea ambayo itarahisisha upatikanaji wa huduma zake kwa wateja wa mjini hapo ambao awali walikuwa hawana namna ya kupata huduma za moja kwa moja kutoka kwenye kampuni hiyo ya simu.
Uzinduzi huo umehudhuriwa na Mkuu wa Wilaya wa Songea Mjini Bw. Joseph Mkirikiti, ambaye ameipongeza Tigo kwa hatua yake ya kuzidi kusogeza karibu huduma zake kwa watu wa Songea.
“Pamoja na utatuzi wa kero za mawasiliano naamini ya kwamba duka hili jipya litakuwa kama kituo cha kutoa huduma mbali mbali ambazo wateja wenu wa Songea watakuwa wanahitaji kutoka kwenu kila siku,” alisema Mkirikiti.
Bw. Mkirikiti alisema kwamba huduma mbalimbali za mawasiliano zitolewazo na kampuni ya simu ya Tigo kama vile kupiga simu, kutuma SMS, mtandao wa Intaneti pamoja na huduma ya kutuma na kupokea fedha, zimekuwa kichocheo kikubwa katika kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini. “Aidha huduma hizi zimeleta mageuzi chanya katika ufanyaji biashara na kuinua hali ya maisha ya maelfu ya Wanasongea na mamilioni ya watanzania kwa ujumla,” alisema.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Tigo Nyanda za Juu Kusini Bw. Jackson Kiswaga, amesema tawi hilo ambalo linalopatikana Songea mjini mtaa wa Shafi Bora linatarajia kuwahudumia wateja wapatao 150 kwa siku kwa kuwapa huduma mbali mbali za Tigo zikiwemo huduma ya kuunganishiwa intaneti, usajili wa laini za simu, Tigo Pesa na huduma maalum za simu za kisasa (“Smartphones”).
“Duka hili lina manufaa makubwa kwa wateja kwa sababu limeleta huduma zetu karibu zaidi kwao. Pia linapatikana sehemu nzuri kibiashara kiasi kwamba litavutia hata wateja kutoka wilaya zingine na maeneo jirani kama Mbinga, Namtumbo, Tunduru Songea vijijini na Nyasa,”alisema Kiswaga.
Duka hili linatoa huduma nyingine maalum zikiwemo uuzaji wa bidhaa mbali mbali kama simu za kisasa ambapo mteja anaruhusiwa kuzijaribisha kabla ya kununua. “Hii inamuwezesha mteja kufanya uamuzi sahihi katika kuchagua na kununua bidhaa inayokidhi mahitaji yake.”
Tawi la Songea linafikisha jumla ya maduka yanayoendeshwa na kampuni ya Tigo nchini kufikia 40. Kwa mujibu wa Kiswaga, kampuni hiyo ina mipango ya kufungua maduka mengine mengi zaidi katika sehemu mbali mbali nchini.