Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

RC GALAWA AHIMIZA WANANCHI KUJIUNGA NA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Galawa akifungua mkutano wa siku ya wadau wa Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA) ambapo Lengo la mkutano huo ilikuwa ni kuchukua maoni yao na kuwaeleza jinsi TIKA inavyofanya kazi. Kikao hicho kimefanyika leo Machi 28, 2014 katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe.
---
Na Mwandishi Wetu, Korogwe

MKUU wa Mkoa wa Tanga, Luteni Mstaafu, Chiku Galawa amesema Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya ya Jamii (CHF) ni mkombozi wa maisha ya wananchi na hivyo kuwataka viongozi mbalimbali kuwa mstari wa mbele kuhamasisha wananchi wao kujiunga nao ili waweze kunufaika na fuksa mbalimbali zinazopatikana kupitia mfuko huo.

Mheshimiwa Galawa alitoa rai hiyo mwishoni mwa wiki wakati akifungua mkutano wa siku ya wadau wa mfuko wa Afya ya Jamii mijini na Tiba kwa Kadi (TIKA) katika halmashauri ya wilaya ya Korogwe mji iliyohudhuriwa na madiwani, watendaji wa halmashauri wakiwemo wananchi pamoja na maafisa wa mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya Taifa na mkoa wa Tanga.

Alisema bima hizo zina umuhimu mkubwa kwa sababu zinaifanya huduma ya afya kuwa ya uhakika zaidi na kuwataka wananchi kuacha kutumia njia nyengine zaidi ya kujiunga nayo ili kuweza kupata manufaa yake kwani wataweza kupata tiba wakati wanapokuwa wagonjwa.

Aidha alisema ni vema mfuko huo ufuatilie na kusimamia kwa ukaribu ili kurahisisha kufanikisha zoezi hilo kwa kuona umuhimu wa kutoa elimu juu ya mfuko wa afya ya Jamii (CHF/TIKA) itolewe vya kutosha kwa wananchi wa halmashauri hiyo iwe ya mara kwa mara ili jamii iweze kupata kujua kwa undani faida watakazozipata kwa kujiunga na utaratibu huo.

Alisema lazima kumbukumbu za wananchi watakaojiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF/TIKA) zihifadhiwe vizuri ili kuepusha usumbufu kwa wanachama wenu ikiwemo kuwa na mikutano ya mara kwa mara kati ya watoa huduma,wadau pamoja na viongozi wa mfuko huo ili kuhakikisha wanachama wanapata huduma zilizo bora kwa kusikiliza changamoto zinazowakabili pindi wanapokwenda kupata huduma.

Aidha aliwataka kuhakikisha kuwa mfuko huo unakuwa ni ajenda ya kudumu katika vikao vyenu vyote vya maamuzi na fedha zinazopatikana kupitia mipango mbalimbali ya uchangiaji kwenye sekta ya afya yaani asilimia 67 ya fedha zote zitumike kwa ajili ya kununulia dawa kwa wanachama watakaojiunga wapate kuona faida ya matumizi ya fedha wanazochangia ili wananchi wasikatishwe tamaa kwa matumizi mabaya ya fedha zao.

Aliongeza kuwa katika mkoa wa Tanga kuna wilaya ambazo zilishaanza mpango huu wa kuchangia kabla ya kuugua ambapo mkoa mzima una jumla ya kaya zinapatoz 438,277 kati ya kaya hizo ni kaya 93,503 pekee zimejiunga na CHF/TIKA mpaka kufikia desemba mwaka 2013 na hiyo ni sawa na asilimia 21.3.

Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa,Meneja wa Mfuko wa Bima ya Afya Mkoa wa Tanga(NIHF) Ally Mwakababu alisema mwaka 2009 mfuko wa Bima ya Afya ulikabidhiwa jukumu la kuendesha shughuli za mfuko wa Afya ya Jamii(CHF) ambao halmashauri 69 zilikuwa zinaendesha.

Alisema wakati bima hiyo inaanzishwa serikali ilikuwa imelipa tshs. 800, 000,000 kama tele kwa tele kwa halmashauri zilizojiaandikisha kaya ambapo kwa sasa kufikia February 2014 ni tshs. Bilioni 4.7 zilikuwa tayari zimeshalipwa.

Mwakababu aliongeza kuwa kwa mwaka wa fedha 2013/2014(Julai-February 2014) mfuko huo umelipa shilingi milioni 753 ili kufikia jamii ambapo tayari wameshafungua ofisi kila mkoa ikiwemo Tanga na sasa mfuko mwaka huu unafungua ofisi katika mikoa mwengine iliyoanzishwa.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>