Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma itakayowawezesha wahitimu wa vyuo mbalimbali nchini kurejesha mikopo yao kupitia huduma ya Airtel Money kulia pichani ni Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu Bwana Juma Chagonja
---
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na Bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu (HESLB) imeanzisha mapinduzi ya malipo ya kielectoniki kwa kuwawezesha watumiaji wa huduma ya Airtel Money kulipia mikopo ya elimu ya juu kupitia huduma ya Airtel money
Ushirikiano huo kati ya Airtel na HESLB unawawezesha wahitimu wa masomo ya juu katika vyuo mbalimbali nchini kuweza kulipia mikopo yao kwa urahisi kupitia huduma ya Airtel Money na hivyo kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mikopo hiyo
Akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo, Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde alisema” tumewawezesha kupitia huduma yetu ya Airtel money wateja wetu kuweza kulipia mikopo yao ya elimu ya juu inayotolewa na bodi ya mikopo ya elimu ya juu kirahisi wakiwa majumbani mwao. Tunawahakikishia wateja wetu huduma bora, salama, ya uhakika yenye viwango vya gharama nafuu na inayopatikana mahali pote nchini kupitia mawakala zaidi ya elfu 35,000 walionea nchini.
Huduma hii ni ya haraka na nirahisi kutumia, sasa wateja hawana haja ya kusubiri kwenye mistari muda mrefu kufanya malipo, wanachotakiwa ni kufanya muamala rahisi kwa kupitia simu zao kulipa na kupata uthibithisho wa malipo ndani ya sekunde chache
Ili kupata huduma hii mteja anatakiwa kupiga *150*60# na kuunganishwa na orodha ya Airtel Money kasha kuchagua namba 5 kufanya malipo, alafu chagua namba 8 kupata huduma zinginezo kisha kuandika neno HESLB , ingiza kiasi cha pesa, kumbukumbu namba na namba ya siri kufanya malipo aliongeza mmbando
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu Bwana Juma Chagonja alisema”hii imekuja wakati muafaka ambapo baadhi ya waliofaidika na mikopo hii muda wao wa kurejesha malipo ya mikopo yao umekwisha, kwa kupitia huduma hii ya kulipia kwa Airtel Money hakutakuwa na haja ya watu kutembea umbali mrefu na kupanga foleni katika mabenki ili kulipia, tunaleta kwa wateja wetu urahisi wa malipo na njia mbadala ya kurejesha mikopo yao kwa wakati na kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mikopo hiyo.
Chagonja aliongeza kwa kusema kwa kupitia huduma hii ya Airtel Money sasa wateja wetu wataweza kulipa mikopo yao kirahisi wakati wowote mahali popote masaa 24 siku 7 kwa wiki.