Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

WAZIRI MAKUFULI AMFAGILIA JK

$
0
0
Na Mwandishi Wetu, Handeni, Tanga.

WAZIRI wa Ujenzi Dkt. John Magufuli amesifu jitihada zinazofanywa na Rais Jakaya Kikwete ambazo zimewezesha kujenga barabara kwa kiwango cha lami zaidi ya kilomita 11,000 na kuwazidi marais walimtangulia, kwani barabara alizozikuta tangu enzi za mkoloni ni kilomita 7,000.
 Aliyasema hayo wakati wa sherehe za ufunguzi wa barabara ya Mkata- Handeni- Korogwe kwa kiwango cha lami ya kilomita 119 uliofanyika na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dokta Jakaya Mrisho Kikwete juzi na kuongeza kuwa barabara hizo zimejengwa kwa fedha za ndani.

Alisema tokea enzi za mkoloni hadi Rais Kikwete anaingia madarakani alikuta barabara za kiwango cha lami kilomita 7,000, lakini tangu ameingia madarakani yeye miaka nane amejenga barabara kwa kiwango cha lami zaidi ya kilomita hizo kitendo ambacho kitaharakisha maendeleo kwa wananchi.
 Awali akizungumza katika ufunguzi wa barabara hiyo,Mtendaji Mkuu wa
Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Mhandisi Patrick Mfugale alisema kazi ya ujenzi wa barabara ya Mkata hadi Handeni imekamilika Desemba 23,2012 na barabara ya Korogwe- Handeni imekamilika Julai 30,2013.
 Mhandisi Mfugale alisema Kampuni ya SINOHYDRO Corporation kutoka china ilishinda zabuni ya ujenzi wa barabara ya Mkata- Handeni kwa gharama y ash. Bilioni 57.3 bila ongezeko la thamani (VAT).

Lakini pia kampuni hiyo iliweza kushinda zabuni ya ujenzi wa barabara ya Handeni Korogwe kwa gharama y ash. Bilioni 63.1 bila ongezeko la thamani (VAT), lakini hadi sasa kampuni hiyo imelipwa sh. Bilioni 25.8 kwa barabara ya Mkata- Handeni.
 Aliongeza kuwa hadi sasa mkandarasi kwa barabara ya Handeni- Korogwe tayari alishalipwa sh. Bilioni 39 na Mhandisi Mshauri hadi sasa amelipwa sh. Bilioni 4.5. Lakini pia wananchi wa Mkata- Handeni wamelipwa fidia sh. Bilioni 1.8 na Handeni Korogwe wamelipwa sh. Bilioni 1.4.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

Trending Articles