Wazee wa Mtwara wakishangaa kupigwa picha mara baada ya kuwasili nje ya Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo...
Wazee wa Mtwara wakijipanga kuingia katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo...
Wanahabari wakifuatilia mkutano huo.
Katibu wa Wazee wa Mtwara Bw. Seleman Madem ambaye aliongozana na Wazee wa Mtwara kuja jijini Dar es Salaam kuongea na vyombo vya habari juu ya sakata la gesi. Wazee hao ambao wametoka katika umoja unaoshirikisha vyama mbali mbali vyasiasa ikiwemo ABC, APP NA MAENDELEO, CHADEMA, DP, NCCR MAGEUZI, SAU, TLP na UDP. Bw. Mademu alisema kuwa wananchi wa Mtwara wanadai kuwa pamoja na yote hayo kufanyika wao mpaka sasa hawajashirikishwa. Wanamtwara wanasema kuwa hawakuwa na dhamira mbaya ya kuandamana bali ilikuwa ni kuishinikiza serikali juu ya sakata la gesi.
Pia waliviasa vyama vya siasa kujichukulia umaarufu binafsi kwa ajenda ya Gesi, ambao kauli mbiu yao unasema, 'Gesi kwanza Vyama baadae'. Pia walipinga vyombo vya siasa kuripoti vibaya suala la Mheshimiwa Jemsi Mbatia kuwa hakushushwa jukwaani na wanasema mkutano uliisha kwa amani.
Mwenyekiti wa CHAUMA mkoa wa Mtwara Bibi Fatuma Selemani ambaye alikuwa ni mmoja ya wazee waliokuja kuongea na waandishi jijini Dar es Salaam akitilia mkazo suala la Gesi. Wazee hao walikuja jijini Dar es Salaam kuongea na waandishi wa Habari ili kuweza kuishinikiza serikali isiisafirishe gesi ya Mtwara kuja Dar es Salaam.
Jambo ambalo lililoshangaza baada ya Mtandao wa Kajunason Blog kufanya uchunguzi wake ilibaini kuwa wazee hao waliletwa na Chama cha NCCR Mageuzi kinachoongozwa na Mh. James Mbatia kuja jijini Dar es Salaam kumsafisha. Kwa mujibu wa barua iliyopatikana ndani ya ofisi za ukumbi huo zilionyesha kuwa Ukumbi huo ulikodiwa na Chama hicho jambo lililoonyesha wazi kuwa wazee hao waliletwa na chama hicho japo wenyewe walikataa katu katu kuwa wameuza kuku, mbuzi zao kuja jijini Dar kuzungumzia sakata la gesi jambo ambalo si kweli. Kwa vile mwanzo wazee hao waliongelea swala la gesi na kupinga kuwa Mh. Mbatia eti hakupigwa wala kufanyiwa fujo mara baada ya kwenda mjini Mtwara kufanya mikutano yake ya ndani.
Waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini. Kama ulipitwa na Sakata la Mheshimiwa James Mbatia huko Mtwara... Soma habari hii iliyoandikwa na Gazeti la mwananchi ilikuwa na kichwa cha bari kilichosema, 'Sakata la gesi Mtwara, Mbatia na wabunge wake hatiani' Link hii: http://www.mwananchi.co.tz/habari/Siasa/-/1597332/1664928/-/bop66iz/-/index.html