Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

RAIS JAKAYA KIKWETE KUHUTUBIA BUNGE MAALUM LA KATIBA JUMATANO 19, 2014

$
0
0
Na Magreth Kinabo- Maelezo, Dar es Salaam.

Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kulihutubia Bunge Maalum la Katiba Machi 19,mwaka huu.

Kauli hiyo imetolewa leo na Mwenyekiti wa bunge hilo Samwel Sitta mjini Dodoma baada ya kusitisha shughuli za kuapisha wajumbe wa bunge hilo.

Mwenyekiti huyo alisema Rais Kikwete atalihutubi bunge hilo mara baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiiko ya Katiba Jaji Joseph Warioba kuwasilisha rasimu ya pili ya Katiba mpya Machi 17, mwaka huu majira ya saa10.00 jioni.

Aidha Sitta aliongeza kuwa wajumbe wabunge hilo ambao hawajaapishwa wataendelea kuapishwa Machi 17, mwaka huu mara baada ya kuanza kwa kikao cha bunge hilo kuanza saa 3:00 asubuhi.

Alifafanua kuwa wajumbe wa bunge hilo wanatarajiwa kupewa semina ya juu ya mabadiliko ya katiba mpya kutoka ujumbe maalum nchini Kenya Machi 8, mwaka huu.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

Trending Articles