Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

ASKARI POLISI WATAKIWA KUBADILIKA ILI KUJENGA HESHIMA ZAO NA TAASISI

$
0
0
CP Mussa Ali Mussa, akitoa maagizo kwa Wakaguzi wa Polisi wanaoshiriki katika mafunzo ya Miundombinu ya Maadili na mikakati ya kudhibiti rushwa yanayofanyika mjini Dodoma.
Pix namba A9968. Afisa Habari Mkuu wa Jeshi la Polisi Zanzibar Inspekta Mohammed Mhina, katikati akiwaelekeza jambo waandishi wa Habari wa Jeshi la Polisi walioshiriki katika mafunzo ya Miundombinu ya Maadili na mikakati ya kupambana na rushwa. kushoto ni Insp. Dickison Gibeshi na kulia ni Sgt Shabani Msangi,
Wakaguzi wa Polisi kutoka mikoa mbalimbali nchini wanaoshiriki mafunzo ya miundombinu ya maadili na mikakati ya kupambana na vitendo vya rushwa wakimsikiliza Kamishna wa Polisi Jamii nchini CP. Mussa Ali Mussa, wakati akitoa mada juu ya umuhim wa Polisi Jamii.
---
Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi -Dodoma

DODOMA, JUMAPILI MACHI 16, 2014. Maafisa na Askari Polisi hapa nchini, wametakiwa badili tabia zao kwa kujiepusha na vitendo vya kudai na kupokea rushwa kutoka kwa watu wenye Matatizo yanayohitaji huduma za kipolisi.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Kitengo Ufuatiliaji na Tathimini cha Jeshi la Polisi nchini, Naibu Kamishna (DCP) Mpinga Gyumi, wakati akitoa mada kwa washiriki wa Mafunzo ya kuimarisha Miundombinu ya Maadili na mapambano dhidi ya Rushwa yanayotolewa kwa Wakuu wa Polisi wa Tarafa na Majimbo yanayofanyika mjini Dodoma.

DCP Gyumi, ameonya kuwa Jeshi la Polisi halitamvumilia Afisa ama Askari yeyotw atakayekwenda kinyume na maadili ya Jeshi hilo jambo ambalo amesema limekuwa likipakwa matope.

Akikariri baadhi ya vifungu vilivyomo kwenye kitabu cha miongozo ya Jeshi la Polisi nchini Police General Order (PGO), amesema kitabu hicho kimetoa makatazo kwa Askari Polisi wa vyeo mbalimbali na kutoa maelekezo mazuri yanayofaa kufuatwa na kila Askari Polisi.

DCP Gyumi pia amewakumbusha Maispekta hao pamoja na Maafisa wa ngazi ya juu wa Jeshi hilo kujiepusha na vitendo vya kupokea zawadi kwani kwa kufanya hivyo ni sawa na kuhalalisha rushwa.

Amesema rushwa imekua ikipunguza heshma na uadilifu kwa mtumishi na hivyo kumfanya kushindwa kuheshimu sheria, kanuni, taratibu na kuwafanya baadhi ya watumishi kujilimbikizia mali kwa njia zisizo halali, wizi na ubadhirifu wa mali ya umma.

Amewaonya wale wote wanaojihusisha na matumizi mabaya ya mali za umma kama vile magari, kompyuta, mashine na vitendeakazi vingine kuacha kufanya hivyo kwani matokeo yake ni kuitia serikali hasara.

Amewataka Maafisa na Askari wa ngazi zote kuwa wasafi mbele ya Jamii hali itakayilifanya Jeshi la Polisi kuwa kimbilio la wanyonge na sio kukimbiwa. “ Nawaombeni kila mmoja wenu kutimiza wajibu wake na kuzaliwa upya hata kama anadhani ameshindikana”. Alisema DCP Byatao.

Naye Kamishna wa Polisi Jamii nchini CP Mussa Ali Mussa, amewataka Mainspekta hao kuhakikisha kuwa wanaondokana na vitendo vya kudai na kupokea rushwa ili wawe mfano bora kwa jamii na Askari waliochini yao.

Awali Mkuu wa Kitengo cha Maadili na Nidhamu cha Jeshi la Polisi nchini SACP Patrick Byatao, alisema hadi sasa, zaidi ya Polisi 1,100 wakiwemo Maafisa Wanadhimu wa Polisi wa mikoa, Wakuu wa Upelelezi wa wilaya na wa Usalama Barabarani hapa nchini, wameshanufaika na mafunzo hayo yanayofadhiliwa na Shirika la Misaada la Maendeleo la nchini Uingereza (DFID).

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>