Muigizaji Rich Rich ambaye ni mmoja ya jaji katika shindano la kusaka vipaji vya uingizaji (Tanzania Movie Talent) akiongea na waandishi wa habari wakati wa kutangaza zawadi wa shindano hilo linalotarajiwa kufanyika katika mikoa mbali mbali hivi karibuni. Kushoto ni Meneja Mradi wa shindano la kusaka vipaji (Tanzania Movie Talent) Joshua Moshi, Meneja Masoko wa Kampuni ya Proin Promotions, Evance Stephen.
Waandishi wa habari wakiendelea na kazi.
Meneja Mradi wa shindano la kusaka vipaji (Tanzania Movie Talent) Joshua Moshi, akielezea namna vijana watakavyopatikana. Pembeni yake ni Meneja Masoko wa Kampuni ya Proin Promotions, Evance Stephen na Muigizaji Rich Rich ambaye ni mmoja ya jaji katika shindano la kusaka vipaji vya uingizaji (Tanzania Movie Talent).
---
---
Kampuni ya Proin Promotions Limited ambao ni watengenezaji, wauzaji na wasambazaji wa Filamu za Kitanzania Inakuja na Kali ya Mwaka 2014 katika kuhakikisha inasaka vipaji vya uigizaji Tanzania ili kuhakikisha inaleta mabadiliko na kuibua vipaji katika tasnia ya filamu nchini ambayo inaonekana imesahaulika kabisa kwa kuleta Shindano la Kusaka Vipaji vya Filamu Tanzania lijulikanalo Kama TANZANIA MOVIE TALENTS (TMT) ambapo litazunguka katika kanda sita Tanzania katika Kushindanisha vijana wenye vipaji vya kuigiza na hatimaye Kila mkoa utatoa washindi wa tatu na watasafirishwa hadi Jijini Dar Es Salaam kwa ajili ya raundi ya pili ya mchujo na hatimaye kufanyika Fainali Kubwa ambapo Mshindi wa Kwanza Atajishindia Kitita Cha Shilingi Milioni 50 za Kitanzania.
Kanda ambazo zitazungukiwa na timu nzima ya Proin Promotions Limited katika kusaka vipaji vya uigizaji ni Kanda ya ziwa (Mwanza na Kigoma),Kanda ya Kaskazini (Arusha), Kanda ya Kati (Dodoma), Kanda ya Nyanda za Juu Kusini (Mbeya), Kanda ya Pwani (Dar es Salaam), Kanda ya Kusini (Mtwara) ambapo katika kila kanda watatoka washindi watatu na watano katika kanda ya pwani ambao watakuja Dar-es-salaam kwa ajili ya raundi ya pili ya mchujo.
Raundi ya pili itakuwa na jumla ya watu 23.Kisha kutakuwa na fainali kubwa kabisa ya Kumsaka mshindi wa TANZANIA MOVIE TALENTS ambayo itafanyika Katika Jiji La Dar na Mshindi wa Kwanza kunyinyakulia Kitita cha Shilingi Milioni 50 za kitanzania(50,000,000/=).
Washindi kumi bora watafanya filamu ya pamoja na Mshindi wa Kwanza atakuwa chini ya Uangalizi wa Kampuni ya Proin Promotions Limited ambapo atakuwa akifanya kazi na Kampuni hiyo Mahiri katika Kutengeneza, kusambaza na kuuza Filamu za Kitanzania.
Proin Promotions Limited ambao ni watengenezaji wa Filamu ya Foolish Age, Figo, Long Time, Kigodoro na Kitendawili wanatarajia kuanza zoezi la hili Aprili 1 mwaka huu katika kanda ya ziwa mkoa wa Mwanza. Watakao ruhusiwa kushiriki katika shindano hili ni vijana wa kitanzania ambao hawajawahi kufanya filamu yoyote wenye umri kuanzia miaka 14 na kuendelea. Filamu ya washindi kumi bora itatengenezwa na kusambazwa na Kampuni ya Proin Promotions Limited.
Pia Proin Promotions Limited inawataka vijana wote wenye umri kuanzia miaka 14 na kuendelea ambao wanahisi wana vipaji vya uigizaji kujitokeza kwa wingi katika mikoa hiyo iliyotajwa pindi zoezi hilo litakapowasili katika Mkoa husika.
Zoezi hili la kusaka vipaji vya uigizaji Tanzania linatarajiwa kuanza mwanzoni mwa Mwezi wa Aprili 1 mwaka huu katika kanda ya ziwa mkoa wa Mwanza na tunaomba vijana ambao wanahisi wana vipaji kuweza kujitokeza kwa wingi katika shindano hilo pindi tu tutakapofika katika mkoa wa kanda husika na Shindano hili litaendeshwa kwa uwazi na bila upendeleo kama mashindano mengine yanavyolalamikiwa na watanzania. alisema Mratibu wa Shindano hilo la Tanzania Movie Talents (TMT) kutoka Proin Promotions Limited Bw Joshua Moshi.
Aliongezea kwa kusema Tunatarajia Shindano Hili la Kwanza Kabisa Kutokea Nchini Tanzania Litakuwa ni sehemu ya kuleta Mabadiliko haswa katika tasnia ya Filamu nchini Tanzania na ni shindano litakalokuwa endelevu.
Ili kuweza kufahamu Mahali na Muda ambapo zoezi hili litafanyika katika Mkoa husika tunaomba wadau wote Kuweza Kupenda ukurasa wetu wa facebook ambao unapatikana katika kiunganishi hiki cha http://www.facebook.com/tztmt na kuendelea kusikiliza vyombo mbalimbali vya habari na Mitandao ya Kijamii kama vile Instagram (tmt_tz)
Twitter (tmt_tz) na kufuatilia tovuti yetu ya http://www.proinpromotions.com na pia Lukaza Blog inayopatikana kwa kiunganishi hiki cha http://www.josephatlukaza.com ambapo Watanzania wote wataweza kufahamu kila kinachoendelea kuhusiana na Shindano hili Kubwa la Tanzania Movie Talents (TMT) ambalo ni la kwanza na la aina yake kabisa kutokea nchini Tanzania.