Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

USAHIHISHAJI WA MITIHANI SHULE ZA MSINGI KWA KUTUMIA KOMPYUTA WAPATAMAFANIKIO JIJINI DAR ES SALAAM.

$
0
0
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es salaam Bi. Theresia Mmbado akifunga mafunzo ya siku 3 ya matumizi ya Fomu za OMR kwa walimu wakuu 254 wa shule za Msingi za mkoa wa Dar es salaam yaliyofanyika katika shule ya Sekondari Shaaban Robert.
Picha na 2. Afisa Elimu wa mkoa wa Dar es salaam Bw. Raymond Mapunda akitoa ufafanuzi kwa walimu wakuu wa shule za Msingi za mkoa wa Dar es Salaam kuhusu namna mkoa ulivyojipanga kutatua changamoto za elimu.
Baadhi ya Walimu wakuu wa shule za Msingi jijini Dar es salaam wakifuatilia michango mbalimbali iliyokuwa ikiwasilishwa kuhusu maboresho ya matumizi ya mfumo wa OMR. Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.
---
Na Aron Msigwa – MAELEZO.
5/3/2014, Dar es salaam.

Matumizi ya mfumo mpya wa kufanya mitihani kwa kutumia karatasi maalum za OMR (Optical Mark Reader) na usahihishaji wa mitihani hiyo kwa njia ya kompyuta umeonyesha mafanikio jjini Dar es salaam mara baada ya vitendo vya udanganyifu na wizi wa mitihani ya shule ya msingi kudhibitiwa.



Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es salaam Bi. Theresia Mmbado ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es salaam wakati akifunga mafunzo ya siku 3 ya matumizi ya Fomu za OMR kwa walimu wakuu 254 wa shule za Msingi za mkoa wa Dar es salaam.

Amesema matumizi ya karatasi maalum za OMR yamefanikiwa kudhibiti vitendo vya udanganifu na kurahisisha utoaji wa matokeo na kuipunguzia serikali gharama ya kusahihisha mitihani hiyo ambayo hapo awali ilikua ikichukua muda mrefu na kuchelewesha matokeo ya wanafunzi.

“ Nikiwa mwenyekiti wa usimamizi wa mitihani wa mkoa wa Dar es salaam kwa mwaka 2013 nakiri kuwa mkoa wetu umepata fomu mafanikio makubwa katika usimamizi wa mitihani na kupunguza udanganyifu kwa sababu ya hizi” amesema.

Amesema kuwa zipo changamoto ambazo mkoa unaendelea kuzifanyia kazi ili kurahisisha matumizi ya mfumo huo kwa walimu na wanafunzi kuwa ni pamoja na uchakavu wa meza za kufanyia mitihani ambazo huchangia karatasi za OMR kujikunja na wakati mwingine kuchakaa na kupoteza sifa ya kusahihishwa na kompyuta.

Pia ameeleza kuwa ipo changamoto ya baadhi ya shule binafsi ambazo walimu wakuu wake wamekwishapatiwa mafunzo hayo lakini wamekuwa wakihama kutoka eneo moja hadi jingine hivyo kuathiri mafunzo kwa wanafunzi na waalimu kuhusu namna ya kuweka vivuli kwenye karatasi hizo.

“ Natoa rai kwa baadhi ya wamiliki na walimu wakuu hasa wa shule binafsi wasiotoa ushirikiano na kushindwa kuleta walimu wao katika mafunzo kama haya tutaanza kuwafuatilia, ikibidi watumie gharama zao wenyewe kuhakikisha walimu wao wanapata mafunzo haya muhimu kwa mustakabali wa taifa letu na maisha wanafunzi wetu” amesisitiza.

Amewataka wakuu hao waliopata mafunzo hayo kuwa mabalozi kwa wengine ambao hawakupata mafunzo hayo kwa kuonyesha utofauti ili gharama iliyotumika wakati wa mafunzo hayo iweze kuzaa matunda na kuleta faida kwa wananchi.

Amesema Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA) limekwishatoa kiasi cha shilingi milioni 138 kwa ajili ya mafunzo ya walimu wa kuendelea kusimamia zoezi la matumizi ya fomu za OMR katika uendeshaji wa mitihani ya kumaliza elimu ya msingi na kuongeza kuwa takribani walimu 7,105 wameshapatiwa mafunzo kwa ngazi ya kata.

Kwa upande wake Afisa Elimu wa mkoa wa Dar es salaam Bw. Raymond Mapunda ameeleza kuwa mkoa wa Dar es salaam licha ya kukabiliwa na changamoto mbalimbali umekuwa ukifanya vizuri katika matokeo ya shule za msingi kitaifa.

“Mkoa wa Dar es salaam ni miongoni mwa mikoa inayopokea wanafunzi wengi kila mwaka mathalani mwaka 2013 tumesajili wanafunzi 63,000 na mwaka huu 2014 tunatarajia kupokea wanafunzi 68,000 kiwango ambacho kinazidi kupanda kilinganishwa na miundombinu iliyopo”

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>