Mwelimishaji wa masuala ya lishe kutoka mradi wa USAID Tuboreshe Sara Luzangi, akiongea na wanafunzi wa shule za msingi wilayani Babati mkoani Manyara, juu ya umuhimu wa matumizi ya vyakula vilivyowekwa virutubishi katika kampeni za kutoa elimu hiyo zinazoendelea katika wilaya mbalimbali za hapa nchini.
Mwelimishaji wa masuala ya lishe kutoka mradi wa USAID Tuboreshe Sara Luzangi, akiongea na wanafunzi wa shule za msingi wilayani Babati mkoani Manyara hawaonekani pichani, juu ya umuhimu wa matumizi ya vyakula vilivyowekwa virutubishi katika kampeni za kutoa elimu hiyo zinazoendelea katika wilaya mbalimbali za hapa nchini.
Wanafunzi wa shule za msingi wakipata burudani ya mafunzo ya lishe kutoka waelimishaji kutoka mradi wa Tuboreshe Chakula unaoendeshwa na mradi wa USAID Tuboreshe Chakula wilayani Babati mkoani Manyara leo
Wanafunzi wakigawiwa vipeperushi vyenye maelezo ya virutubishi kutoka kwa waendesha kampeni wa mradi wa Usaid Tuboreshe Chakula katika kampeni inayoendelea wilayani Manyara iliyozinduliwa jana wilayani humo
Afisa utawala wa Wilaya ya Babati, Bwana Mshamu akiongea na wadau kutoka sekta mbalimbali wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuongeza virutubishi kwenye chakula inayoendeshwa na mradi wa USAID Tuboreshe Chakula .Kampeni hizo zinaendela wilayani humo leo
Waendeshaji wa kampeni ya kuongeza virutubishi katika chakula kutoka mradi wa USAID Tuboreshe Chakula wakiendesha kampeni ya umuhimu wa virutubishi kwa wanafunzi wa shule za msingi wilayani humo leo