Promota wa ngumi za kulipwa, Jay Msangi amemshutumu RAIS wa Oganaizesheni ya Ngumi cha Kulipwa (TPBO), Yassin Abdalla 'Ustaadh ' ambaye ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Shirikisho la Ngumi za Kulipwa la Afrika ya Mashariki na Kati (ECAPBA) kuwa ndiye mchawi wake ambaye amesababisha kuvunjika mpambano wa tarehe 8 Feb 2014.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Msangi alisema kuwa amesikitishwa sana na barua ya Baraza la Michezo Tanzania maana madai yote hayo yalepelekwa na Yassin Abdalla ambaye kwa upande wake yeye alipoandaa Mpambano alilipa ada zote ila anashangaa anapochafuliwa.
"Mchawi wangu ni Yassin Abdalla wala sifichi lolote maana yeye ndiye aliyepiga fitina kwa BMT na wakasimamisha mpambano wangu uliokuwa ufanyike, Feb 8, mwaka huu, napenda niseme kuwa mimi sitakufa moyo na wala siogopi japo nimeingia hasara... Hawa ni wachawi wanaotaka kurudisha nyuma mchezo wa ngumi".