Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

HATUMTAKI RAGE AJIONDOE MWENYEWE IFIKAPO JUMAMOSI DEC 7

$
0
0
WANACHAMA wa Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam, wamemtaka mwenyekiti wao Aden Ismail Rage kuachia ngazi ifikapo Desemba 7 mwaka huu, kabla ya wao kufunga safari kumfuata mjengoni mjini Dodoma kwa lengo la kumshinikiza ajiuzulu.

Akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya wenzake, Ramadhan Masoud, mwanachama mwenye Kadi No, 536 Tawi la Mpira Pesa, kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO, jijini Dar es Salaam, mchana huu, akiwa ameongozana na wanachama wenzake wapatao 50 waliofika kwenye ukumbi huo, alisema kuwa sababu kuu ya kumtaka ajiuzulu kwa hiyari yake ni kuchoshwa na ubabe na vituko vya mwenyekiti wao.

Aidha Ramadhan alisema kuwa hawamtaki Rage kwa kile walichodai amekuwa akikiuka Katiba yao na kuwapuuza wanachama wa Klabu hiyo, kila wanapomtaka aitishe Mkutano Mkuu ili kujadili na kutafuta muafaka wa kutatua mgogoro unaoendelea ndani ya Klabu hiyo.

''Kwa kweli tumemchoka na hatumtaki Mwenyekiti wetu na huyo Wambura wake aliyemteua hivi karibuni kutokana na kuvunja katiba na kugoma kuitisha mkutano mkuu, anaonekana anataka kuipelkea pabaya timu yetu''. alisema Ramadhan

Mwezi uliopita Rage alikaidi agizo la Shirikisho la mpira wa miguu TFF, lililomtaka aitishe mkutano mkuu ili kutatua mgogoro unaoendelea ndani ya Klabu hiyo, huku akinukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari akisema kuwa TFF ilichemka kumtaka aitishe mkutano mkuu, na kusema kuwa hawezi kuivunja katiba ya timu yake kwa kufuata maelekezo ya TFF.
Wakizungumza na mtandao huu baada ya kumalizika kwa mkutano huo baadhi ya wanachama hao, walisema kuwa wanamsihi Rage kufanya hivyo kabla ya wao kufunga safari na kwenda kumhaibisha kwa wabunge wenzake huko mjini Dodoma.

''Unajua hadi unaona tumejikusanya hivi kwa umoja wetu ni kwamba tunamaanisha tumechoshwa kweli na vituko vyake na tunahitaji mabadiliko ili tuweze kufanya vizuri katika mzunguko wa pili na hata katika mashindano mengine, hatuhitaji mpira wa siasa.'' alisema mmoja wa wanachama hao..

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>