Vibaka wawili wanusurika kifo baada ya kupokea kichapo cha mbwa mwizi baada ya kukamatwa wakiwa wametega mtego wao katika daraja la Mlalakua jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita wakati wa shindano la EBSS. Kajunason Blog baada ya kufika eneo la tukio mwishoni mwa wiki iliyopita majira ya saa 3usiku ilishuhudia vibaka hao wakiadabishwa na ilipohoji iliambiwa walikuwa wametega pikipiki yao wakitaka kukwapua simu ambayo jamaa alikuwa akiongea nayo huku akiwa kwenye gari ndipo gari la mbele lilipofanikiwa kugonga piki piki na jamaa wakadondoka na kuanza kupata kipigo.
Mmoja wa mashuhuda wa mtego mzima alisema vijana hao wakati wa jioni huwa wakitembea na pikipiki na kuwavamia watembea kwa miguu na kuwapora vitu vyao lakini vile vile huwapora hata watu waliopo kwenye magari. (Pichani ni kijana akijaribu kujielezea mbele ya wananchi waliokuwa na hasira kali mata baada ya kamera ya Kajunason Blog kutinga eneo la Tukio ndipo wananchi hao walipunguza munkali wa kuwapa kichapo).
Hapa kibaka huyo akipokea kichapo kitakatifu... wakati akijitetea
.... kibaka akiwa amedondoka
Pikipiki iliyokuwa ikitumiwa na vibaka kwa ajili ya kupora
Hakika usiombe kukutana na wananchi wenye hasira kali ambao walishawahi kuonja machungu ya kuibiwa mali zao, hapa ilikuwa ni piga nikupige
Wakijaribu kumuhoji huku akipokea kichapo....
Kila mmoja alijaribu kutoa machungu yake kwa kutoa kichapo...
Baada ya kuwa dereva wa pikipiki (mwenye koti) kukimbia alifanikiwa kukamatwa baada ya wananchi hao kutoa tamko la kuiteketeza pikipiki kwa moto ndipo jamaa alipojitokeza...