Baada ya usaili wa kumtafuta mrembo wa kurithi taji la Miss Universe Tanzania
kumalizika, kambi ya warembo kwa ajili ya kinyang’anyiro cha kumtafuta mrithi wa taji la Miss Universe Tanzania 2013 imeanza rasmi.
Kambi hii ambayo imejumuisha warembo 15 kutoka mikoa nane ya Tanzania itakaa kwa muda wa wiki moja katika hotel ya Urban Rose kabla ya kumpata mshindi siku ya
fainali ambapo itakuwa tarehe 27 mwezi Septemba mwaka huu katika ukumbi wa
Makumbusho ya Taifa.
Ukilinganisha na miaka mingine mashindano ya mwaka huu yatakuwa tofauti kidogo
ambapo ukiondoa kugombania taji kubwa la Miss Universe Tanzania kulikuwa na
washindi wa pili na watatu. Mwaka huu mshindi mwingine atavikwa moja kwa moja taji la Miss Earth Tanzania na Mshindi wa tatu bora ndio atakua runner up.
Warembo watakaochuana kuwania taji hilo ni kama ifuatavyo na mikoa waliyotoka kwenye mabano. Aziza Victoria(Dar es Salaam) , Irene Nsiima (Dar es Salaam), Betty
Boniface(Dar es Salaam), Kundi Mlingwa(Dar es Salaam), Mariam Ngwangwa(Dar es
Salaam) , Consolata Mosha( Mwanza), Agnes Thobias, Dinah David ( mbeya), Upendo
Dickson (Dar es Salaam), Naomi Kisaka(Dar es Salaam), Glady Msemo(Dar es Salaam) ,
Vestina Mhagama(Dar es Salaam) , Angela Lutataza(Dar es Salaam) , Clara Noor(
Mwanza), Sasha Lukiko(Dar es Salaam).
Timu ya Compass Communications ilizunguka takriban Mikoa 8 ya Tanzania kufanya
usahili kwa kila mkoa ili kupata wawakilishi wa mikoani katika kinyang’anyiro hiki.
Mikoa hiyo ni pamoja na Mwanza, Arusha, Mtwara, Manyara, Mbeya, Dodoma,
Kilimanjaro na Dar es Salaam. Jumla ya washiriki 15 wataingia kambini kuchuana
kumpata Mwakilishi wa Tanzania katika fainali za dunia zitakazofanyika nchini
Moscow,Urusi.
Mashindano ya Miss Universe kwa hapa Tanzania yalianza rasmi mwaka 2007 ambapo Tanzania iliwakilishwa na Flaviana Matata na kufanikiwa kuingia katika kumi bora na mwaka 2008 yaliwakilishwa na Amanda Ole Sulul, 2009 yaliwakilishwa na Illuminata
James ambapo mwaka 2010 mrembo Hellen Dausen ndiye aliyepokea kijiti, 2011 Nelly
Alexandra Kamwelu na anayekabidhi taji mwaka 2012/2013 ni Winfrida Dominique.
Mashindano ya Miss Universe yamedhaminiwa na Hifadhi za Taifa (TANAPA), Fastjet,
Mohamed Enterprises (MetL) na Wadhamini wenza(Parters) ni CocaCola, Missie
Popular Blog, Healthy Beauty Clinic, Beauty Point, Sia Couture, Seif Kabelele Blog, AZH Photography.com na Adams Digicom