
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Said Mwema akimkabidhi pikipiki Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar Es Salaam, Naibu Kamishna wa Polisi Suleiman Kova kama ishara ya kukabidhiwa Makamanda wote Tanzania bara na Visiwani ambapo jumla ya Pikipiki 564 zimekabidhiwa kwa ajili ya kuzuia uhalifu kwa lengo la matumizi ya Wakaguzi Tarafa wa Polisi Tanzania bara na Majimbo yote ya Zanzibar, program za Safiri Salama na Usalama wetu kwanza.
Makabidhiano hayo yamefanyika katika makao makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na Makamanda na maafisa mbalimbali wa jeshi hilo.



Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Said Mwema kulia akiwa katika hafla ya makabidhiano hayo makao makuu ya jeshi la polisi jijini Dar es salaam leo asubuhi, katikati ni Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Polisi Paul Chagonja na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar Es Salaam, Naibu Kamishna wa Polisi Suleiman Kova


Maafisa mbalimbali wa jeshi la polisi wakiwa katika hafla hiyo leo asubuhi.

