Mabondia Thomas Mashali wa Tanzania (kushoto) na Benard Mcociech wa Kenya wakitunishiana Misuli baada ya kupima Uzito Dar es salaam jana kwa ajili ya mpambano wao wa Ubingwa wa Afrika Mashariki utakaofanyika leo katika ukumbi wa Frends Corner Manzese
Mtanzania Thomas Mashali na Bernad Mackoliech kutoka nchini wa Kenya wakitambiana mara baada ya kupima uzito leo katika ukumbi wa Friends Conner, Manzese jijini Dar es Salaam.
---
Na Cathbert Angelo, Dar es Salaam.
Kamanda wa polisi mkoa wa Kipolisi wa kinondoni Charles Kenyela anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika pambano la kutetea ubingwa Afrika mashariki na kati kati ya bondia Mtanzania Thomas Mashali na Bernad Mackoliech kutoka nchini wa Kenya Jumamosi katika Ukumbi wa Friends Corner Manzese.
Akizungumza na waandishi wa habari leo wakati mabondia hao wakipima uzito, mratibu wa pambano hilo Aisha Mbegu alisema wameamua kumualika kamanda Kenyela ili kuhakikisha wanatumia nafasi hiyo kutoa Elimu ya Ulinzi shirikishi na kwa kutambua mchango wa jeshi la polisi kudumisha amani katika michezo.
“Jeshi la polisi ni wadau wetu wakubwa katika michezo hasa ngumi na mchango wao umekuwa ukionekana kwani sasa hakuna vurugu zinazojitokeza katika mapambano yeyote ya ngumi yanayofanyika tofauti na Miaka ya Nyuma ambapo Ngumi ilikuwa Watoto hawawezi kwenda kuangalia,” alisema Aisha.
Aisha alisema katika pambano la awali ambalo lilifanyika katika Ukumbi wa Friend Corner hakukuwa na vurugu na idadi ya watoto na wanawake kuangalia ngumi imekuwa ikiongezeka siku hadi siku na hivyo kutoa hamasa kwa wazazi na watoto kupenda mchezo huo.
Mbali na Kenyela Mbunge wa Kinondoni Iddi Azan na Mbunge wa ubungo John Mnyika wamealikwa ili kushuhudia vipaji vya vijana wa kinondoni katika Ngumi.