Mkuu mkoa wa Kigoma,Kanali Mstaafu,Mh Issa Machibya akizungumza machache wakati wa ufunguzi wa Semina ya Fursa kwa vijana zinazopatikana ndani ya mkoa wa Kigoma na kwingineko
Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akimkaribisha mgeni rasmi wa semina hiyo,Mh Issa Machibya wakati wa uzinduzi wa semina ya Fursa,kulia kwake ni msanii mahiri wa kughani mashairi hapa nchini,Mrisho Mpoto ambae pia likuwa ni mmoja wa watoa mada kuhusiana na suala zima la Fursa.
Sehemu ya Meza kuu ikishangilia jambo,kutoka kushoto ni Kaimu Meneja wa NSSF mkoani Kigoma,Bwa.Said Abdallah,Mkuu wa Wilaya ya Uvinza ambae alikaimu pia nafasi ya Mkuu wa wilaya ya Kigoma mjini,Mh.Khadija Nyembo,Mkuu wa Mkoa,Mh.Issa Machibya,Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji kutoka Clouds Media Group,Ruge Mutahaba,Msanii Mrisho Mpoto (haonekani) pamoja na msanii wa muziki wa kizazi kipya,ajulikanae kwa jina la kisanii AY.
Mkali wa kughani mashairi hapa nchini, Mrisho Mpoto akifafanua jambo mbele ya wakazi wa mji wa kigoma, alipokuwa akiielezea mada mojawapo iliyohusiana na fursa mbalimbali.
Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya na mfanyabiashara, Ambwene Yesaya a.k.a AY akitoa ushuhuda wake na mifano mbalimbali katika Semina ya Fursa,kuhusiana na fursa alizozipata na kuzifanyia kazi, na kumpelekea mafanikio aliyonayo mpaka sasa.
Baadhi ya wakazi wa mkoa wa Kigoma wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa semina ya Fursa.
---
Kampuni ya simu za mkononi ya Zantel, leo imetangaza kudhamini semina za kuhamasisha vijana kuchangamkia fursa zilizopo nchini zitazoendeshwa kwenye zaidi ya mikoa 13 kwa kushirikiana na Clouds Media Group.
Semina hizo ambazo zinaenda sambamba na ziara ya kimuziki ya tamasha la Fiesta ambalo mwaka huu litaenda zaidi ya mikoa 13, zinatarajiwa kufanyika siku moja kabla ya tamasha kila mkoa ambao Fiesta inaenda.
Mada zitakazojadiliwa kwenye semina hizo ni pamoja na ubunifu, ujasiriamali, Uongezaji thamani kwenye bidhaa au shughuli yoyote unayofanya pamoja na kujenga ushirikiano, uwekezaji pamoja na lugha.
Akizungumzia semina hizo, Afsa Biashara Mkuu wa Zantel, Sajid Khan, amesema kampuni yake imekuwa msitari wa mbele katika kuwawezesha vijana, na kwa semina hizi wanaamini vijana wengi watapata nafasi ya kuzitambua na kujifunza.
‘Tanzania ina fursa nyingi sana kwa vijana, na sisi Zantel tunaamini nafasi hii itakuwa muhimu kwa vijana kujifunza na kutambua fursa zilizopo kutoka kwa wataalamu mbalimbali’ alisema Khan.
Naye Mkurugenzi wa Utafiti na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba, alisema nchi ya Tanzania ina fursa nyingi lakini tatizo limekuwa ni namna ya kuzitumia fursa hizo.
‘Tumeandaa semina hizi kwa kutambua tatizo kubwa lilipo kwenye jamii yetu, umaskini na ukosefu wa ajira kwa vijana, jambo ambalo semina hizi zitaenda kutatua’ alisema Mutahaba.
Mojawapo wa wazungumzaji kwenye semina hizo atakuwa Mrisho Mpoto, mwakilishi wa mfuko wa hifadhi ya jamii (NSSF), Ruge Mutahaba pamoja na wageni waalikwa mbalimbali.
Kwa mwaka huu semina hizo zimeanzia mkoa wa Kigoma, katika Ukumbi wa Kibo Hall Park, na mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Issa Machibya.