Maoni kutoka kwa mdau wa soka la bongo Bwana Cannon Luvinga,
Mapato ya mechi ya ngao ya hisani kati ya Yanga na Azam yatapelekwa kwa kituo cha watoto yatima cha SOS. Ivi kweli TFF mmepeleka pesa SOS? Watoto ambao wanawafadhiri nje ya nchi na wana miradi mingi endelevu. Kweli tumefika hapa? Dogodogo centre, donbosco na vituo vingi vya yatima ambapo watoto hawana hata ndala wanashare mmewaacha? SOS wanashida gani? Aisee hii dhambi mliyofanya sijui mtaifutaje. Uchaguzi wa TFF uje tuu aisee ndo hiki mlikuwa mnaking'ang'ania ili uchaguzi usifanyike? Ni kigezo kipi kimetumika kuchagua SOS?
Kiukweli toka moyoni SOS wale watoto yatima wanaishi vizuri kuliko hata watoto wa nyumbani. kama mtu anabisha siku aende na watoto wa miaka 5 katika vituo vingine kama viwili then aende na mtoto huyohuyo kutembelea SOS uone mtoto wako anavyong'ang'ania kubaki SOS. yaani mle ndani kwao kupo kama hotelini then ndo pesa eti wamepewa tena. za nini? ili iweje? dhambi tunayojichumia sidhani kama inaweza sameheka kiurahisi. labda kama hawapajui SOS waliletewa tu jina ila kiukweli kuna vituo vya watoto yatima ambavyo vinahitaji msaada. yaani nimeskia hizi taarifa kupitia luninga usiku huu kwakweli nimekosa raha na nimejisikia vibaya sana. au ndo mwenye vingi ataongezewa?.