Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19867

DKT. MWAKYEMBE AWATAKA VIJANA KUIGA MFANO WA FLAVIANA MATATA

$
0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (katika) akieleza jambo kwa Waandishi wa Habari (hawapo katika picha) wakati wa mkutano leo Jijini Dodoma, kulia ni Naibu Waziri Mhe. Juliana Shonza na kushoto ni Mwanamitindo wa Kimataifa Flaviana Matata.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akifafanua jambo kwa Mwanamitindo wa Kimataifa Flaviana Matata(kulia) katika ofisi za Wizara leo Jijini Dodoma.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Juliana Shonza (kushoto) na kulia ni Mwanamitindo wa Kimataifa Flaviana Matata.

Picha/Habari na Loretha Laurence-WHUSM, Dodoma.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amempongeza mwanamitindo wa kimataifa Flaviana Matata kwa juhudi za kusaidia watoto wa kike kupata elimu kwa kuwawezesha vifaa muhimu vya shule ikiwemo ada na madaftari.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma Dkt. Mwakyembe amewataka vijana wa kitanzania kuiga mfano wa mwanamitindo huyo ili kuchangia katika ujenzi wa taifa.

“Nawasihi vijana wengine wenye fursa kama za Flaviana Matata kuzitumia vizuri kwa kuhakikisha jamii inanufaika na mafanikio waliyoyapata” ameongeza Dkt. Mwakyembe

Aidha, aliongeza kwa kueleza kuwa, Mwanamitindo huyo amekuwa ni balozi mzuri katika kupeperusha bendera ya Taifa katika nchi mbalimbali za Ulaya.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza amempongeza Flaviana kwa kuwa mfano bora kwa watoto wa kike kwa jinsi ambavyo amekuwa akisaidia watoto wa kike nchini.

Naye Mwanamitindo wa Kimataifa Flaviana Matata ameleza kuwa mbali na kujishughulisha na mitindo, ameweza kuanzisha kampuni ya Flaviana Matata Foundation ambayo inasaidia kutoa vifaa vya shule, ambapo hadi sasa amefanikiwa kutoa vifaa zaidi ya 5000 katika shule mbalimbali nchini.

Anazidi kueleza kuwa, Taasisi hiyo imefanikiwa kurabati shule mbalimbali kwa kujenga madarasa na kusomesha wasichana 15 ambao wanamaliza kidato cha sita mwaka huu na wengine watano bado wapo shule.

Hata hivyo, Mwanamitindo huyo ameushukuru uongozi wa Wizara kwa jitihada za wazi wanazozifanya katika kusimamia haki za wasanii na hivyo kurudisha hadhi ya tasnia hiyo nchini.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19867

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>