Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19878

DC SHINYANGA AZINDUA RASMI ZOEZI LA KUGAWA VITAMBULISHO VYA TAIFA KWA WANANCHI

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa Josephine Matiro akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa zoezi la kugawa vitambulisho vya taifa (NIDA) kwa wananchi wa halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga. Kushoto ni Naibu Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Agnes Machiya. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Vihatarishi NIDA Makao makuu,Stephen Kapesa - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Vihatarishi NIDA Makao makuu,Stephen Kapesa akizungumzia kuhusu zoezi la utoaji vitambulisho vya taifa.
Maafisa watendaji,madiwani na watumishi mbalimbali wa manispaa ya Shinyanga wakiwa ukumbini.
Naibu Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Agnes Machiya akimkaribisha mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro kuzindua rasmi zoezi la ugawaji wa vitambulisho vya taifa kwa wananchi wa manispaa ya Shinyanga.
Sehemu ya vitambulisho 12,918 vilivyokabidhiwa kwa maafisa watendaji wa kata 17 za manispaa ya Shinyanga watakaokwenda kugawa vitambulisho hivyo kwa wananchi.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa Josephine Matiro akimkabidhi Kitambulisho cha taifa Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Agnes Machiya wakati akizindua rasmi zoezi la kugawa vitambulisho vya taifa (NIDA) kwa wananchi wa halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
Mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga,Geofrey Mwangulumbi akionesha kitambulisho chake cha taifa baada ya kukabidhiwa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa Josephine Matiro akimkabidhi Kitambulisho cha taifa diwani wa kata ya Lubaga Mchungaji Obedi Jilala (CHADEMA).

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19878

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>