Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19890

RAIS WA TFF WAMUOMBA RAIS DKT. MAGUFULI WAMKABIDHI KOMBE LA CECAFA

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) limemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli  kukabidhiwa kombe la CECAFA na vijana wa chini wa miaka 17 ili kuweza kuwapa hamasa vijana hao.

Hilo limesemwa na Rais wa TFF Walaace Karia wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Makao makuu ya Shirikisho hilo.

Karia amesema kuwa,waliweza kuzungumza na Waziri wa Habari,Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe na tayari ameshaandika barua kwenda kwa Rais Dkt Magufuli kwa ajili ya kuweza kumpa taarifa ya hafla hiyo itakayofanyika siku ya Jumamosi Uwanja wa Taifa.

Mbali na hilo TFF wamemuomba Dkt John Pombe Joseph Magufuli kuwa mgeni rasmi katika mchezo Simba SC dhidi ya Kagera Sugar FC utakaopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Mei 19 2018.

Kwa mujibu wa Rais (TFF),Karia, amesema kuwa wamemwandikia barua Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dokta Harrison Mwakyembe yenye ombi la kumuhitaji Magufuli juu ya ugeni huo.

Karia ameeleza kuwa Rais Magufuli atapata wasaa wa kukabidhi kombe la 19 mabingwa wapya wa Ligi Kuu msimu huu wa 2017/18 ambalo wamelipata wakiwa hawajapoteza mchezo wowote msimu huu.

Mbali na Simba kukabidhiwa taji hilo katika mchezo dhidi ya Kagera Sugar, Magufuli atawakabidhi pia vijana wa Serengeti Boys Kombe la CEFACA chini ya miaka 17 walilolitwaa nchini Burundi baada ya kuifunga Somalia kwa maba0 2-0 kwenye mechi ya fainali iliyopigwa Uwanja wa Ngozi, jijini Bujumbura.

Sherehe za Simba na Serengeti Boys zitaanza majira ya saa 8 mchana huku viiingilio vya mchezo huo (Simba SC vs Kagera Sugar) vikiwa ni 15,000 kwa VIP A, 7000 kwa VIP B na C pia 3000 kwa sehemu ya mzunguko.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19890

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>