
Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu ,Sera ,bunge ,kazi vijana ajira na wenye ulemavu Jenista Mhagama amemuagiza kamishana mku wa kazi nchini kuzifutia usajiri kampuni tisa za wakara binafs wa ajira kwa kosa la kubadili anauani za ofisi zao bila kutoa taarifa kwa kamishina wa kazi na kuto kuwasilisha taarifa kwa kamishina wa kazi mara baada ya mikataba ya kazi ya wafanya hao kukamili.
Aidha waziri mhagama amemuagiza kamishina wa kazi kuzifanyia uhakiki wakala zote zinazoendesha shughuli za wakala binafsi wa huduma za ajira hapa nchini ili kuona kama wanatekereza na kuzingatia matakwa ya sheria ya huduma ya ajira namba 9 ya mwaka 1999 na kanuzi zake kupitia tangazo la serikali namba 232 ya mwaka 2014.
Waziri mhagama ametoa agizo hilo mjini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema amechukua uamuzi huo mara baada ya kubaini uwepo wa udanganyigu mkubwa wa mawakala na kuelekeza shughuli hiyo ifanywe na wakala wa huduma za huduma za ajira wa serikali katika kipindi hiki cha mpito wakati serikali ikiendelea na jitihada za kuangali namna ya kuingia mikataba na nchi husiska ili kuwa na uhakika na watanzania wanaokwenda kufanya kazi nnje ya nchi.