Naitwa Mathew Yinza Telles.Nimezaliwa tarehe 08 July 1992.Jina langu la sanaa naitwa Yincas El Legendee Nickname Killerflo.Jina la Yincas limetokana na jina langu la Yinza ambalo idadi kadahaa ya watu wananifahamu kwa jina hilo.Ukiachana na mzik,pia ni mwanafunzi wa chuo kikuu Mzumbe kilichopo Morogoro nachukua Stashahada ya kwanza ya Health Systems Management.Nimemaliza kidato cha nne katika shule ya St. Francis De Sales na kujiunga na shule ya Loyola High School ambapo nilihitimu kidato cha sita na kufanikiwa kufaulu vizuri kwenda chuo kikuu Mzumbe.Katika familia yangu mimi ni mtoto wa pili nikitanguliwa na dada yangu na mdogo wangu wa kike wa mwisho.Napenda sana mpira wa miguu ni mchezaji mzuri na shabiki wa Arsenal FC,pia napenda sana kuskiliza mziki wa dunia nzima kuanzia hapa nyumbani Tanzania na nchi zingine zote duniani.Napenda sana mziki wa HipHop na ni shabiki wa Rapper wa kimarekani anaeitwa Fabolous ’Loso’ na hapa nyumbani namkubali Fid Q na Ngwea..R.I.P bro.
Safari yangu ya mziki nimeanza mwaka 2007 ndipo nilirecord traki ya kwanza iliyoitwa ‘Ishara Ya Ukombozi’ nilikuwa nipo kidato cha pili na nilimshirikisha kaka yangu wa shule aliitwa ‘Culture’ ambae aliniandikia mistari na produza alikua Dizzy Mchizy.Baada ya hapo nikarekodi trak nyingine iliyoitwa ‘Modern Crunk’ na kuifanyia video iliyopata airtime katika baadhi ya station ikiwemo C2C.Pia sikuishia hapo,mwaka 2008 nikarekodi nyimbo nyingine iliyoitwa ‘Niache Niongee’ chini ya produza Dizzy Mchizy ambayo kwa namna moja au nyingine ilifanya watu waanze kunielewa kwamba nina kipaji.Baada ya kufaulu na kuingia kidato cha tano ndipo nikakutana na Dully Sykes na kufanya nae nyimbo pale Dhahabu Records iliyoitwa BELIEVE ME mwaka 2010 lakin bahati mbaya nyimbo haikusogea kutokana na vikwazo mbalimbali ikiwemo shule kunibana.Mwaka huohuo nikapata idea ya kufanya mixtape yangu iliyoitwa EL LEGENDEE 1 ambayo ilikua na nyimbo kama Believe Me,Niache Niongee,Love You,Don’t Go nk.Namshukuru Mungu mixtape watu waliipenda na kunipa moyo wa kukaza zaidi.Mwaka 2011-2012 ilikuwa ngumu kwa mi kufanya mzik kutokana na shule kunibana nilikuwa form6 ila nlifanya nymbo ya ‘Sweetlove’ na kuiweka mtandaoni ambayo ilipata downloads zaidi ya elfu3.Baada ya kumaliza form6 nilifanya video ya nyimbo ‘Imma Getting Em Off’ ambayo ilitazamwa sana YouTube na kupata sana airtime kwa baadhi ya Station hapa nchini.
Kwa sasa nina project ya kufanya Album Yangu itayoitwa ‘The Rise Of The Young Legendee’ na nishafanya baadhi ya nyimbo ambazo pia zipo kama Trailer katika mitandao mfano HulkShare/yincaskillerflo.Baadhi ya nyimbo hizo ni kama Sweetlove,Mr A Mill Swag,Show Me.Pia nimetoa Tshirts za kusapoti hii album ambazo zipo mtaani.Kwa sasa naachia video mbili za nyimbo zangu SATURDAY na R.I.P.Safari hii nimejipanga vilivyo,am ready for the competition,,you gotta get stay ready,,watu wangu wasubiri new flavour kwa industry.Nitakuwa mchoyo wa fadhila nisipowashukuru hawa watu,,Familia yangu inayonisapoti,Dizzy Produza, Yuddy, Dully Sykes na wanangu wa RoyalFAM(makaino, caliross, jose, sonjay, na mtu mzima BigDadi Kimambo) Na watu wangu wote wanaonisapoti mziki wangu kwa namna moja au nyingine... Nawapenda sana. Follow Me SoundCloud/yincaskillerflo... Instagram/yincaskillerflo... HulkShare/yincaskillerflo... YouTube/yincas08… AHSANTE
#Its Western Musik SwagginUp_RoyalF
EMBED CODE TO MY VIDEO TEASER :