Meneja Chapa wa Tigo, William Mpinga (kulia) akizungumza na mmoja wa washindi watatu wa "Miliki Biashara Yako" katika droo ya kwanza ya promosheni hiyo mapema jana. Katikati ni Bi. Chiku Saleh, Mkaguzi kutoka shirika la Bahati Nasibu Tanzania na Husni Seif, Meneja Bidhaa wa Tigo.
Droo ikiendelea...
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakimsikiliza Meneja Chapa a Tigo, William Mpinga, akizungumza na Waandishi wa Habari katika droo ya Miliki Biashara Yako iliyofanyika jana. Anayeonekana meza kuu pia ni Husni Seif, Meneja Bidhaa wa Tigo.
---
Tigo Tanzania imefanya droo yake ya ufunguzi na kupata washindi wake wa kwanza wa promosheni yao kabambe iitwayo “Miliki Biashara Yako” iliyoshuhudia washindi 3 kila mmoja kujishindia Bajaji mpya yenye thamani ya Tsh 6,700,000.
Washindi hao ni Mohamed Ramadhani Mnjori (39) muuza nguo za mitumba mkazi wa Ilala Dar es Salaam , Riziki Lucas Kisemo (36) mjasiriamali mkazi wa makabe Dar es salaam, na Adam Saidi Kalulu (36) mkulima mkazi wa Kiluvya.
Akizungumza katika mkutano na wanahabari waliohudhuria droo hiyo, Meneja Chapa wa Tigo, Bw. William Mpinga aliwapongeza washindi hao na kutoa rai kwa wateja wengine pia kushiriki katika promosheni hiyo.
“Kila mteja wa Tigo anao uwezo wa kujishindia Bajaji moja kila siku kwa muda wa siku 60 kwa kuongeza vocha ya Tsh 1,000 tu kwa siku. Ili kuhakikisha kuwa wateja wengi wanafurahia promosheni hii, mteja hahitaji kuweka vocha ya Tsh 1000 kwa mkupuo mmoja ili kushiriki, anaweza kuongeza salio kidogo kidogo hadi kufikisha kiasi cha Tsh 1000 kwa siku na kuweza kuingia kwenye droo. Vile vile mteja anaweza kuongeza salio mara nyingi awezavyo ili kujiongezea nafasi zaidi ya kujishindia Bajaji. Pamoja na hayo, ili kuwapatia urahisi zaidi wateja, bado mteja anaruhusiwa kuongeza salio pitia namna zote zile ikiwemo Tigo Rusha, Tigo Pesa au kwa vocha ya kawaida,” alisema Mpinga.
“Leo Tigo imetimiza kwa hatua moja jukumu letu tulionao katika kuboresha na kugusa maisha ya Watanzania, kwa kuwapatia nafasi ya kumiliki biashara yao wenyewe kupitia promosheni hii ya “Miliki Biashara Yako”. Hii ni nafasi yakipekee ambapo wateja wetu wanapatiwa fursa ya kuwa wajasiriliamali, kujipatia kipato, kutoa ajira, pamoja na kutoa huduma ya usafiri wenye gharama nafuu kwa jamii.”
Promosheni hii inayalenga kuwainua wateja wake kiuchumi kwa kuwapatia fursa ya kushinda usafiri wa Bajaji 60 kwa muda wa miezi miwili ambapo kila siku mteja atajishindia Bajaji moja.
“Tunaamini kwamba promosheni hii itawapatia wateja wetu sababu nyingine yakutabasamu. Wateja 60 watakaopatikana washindi watajinyakulia Bajaji mpya kabisa ambapo wataweza kuzitumia kuanzisha biashara zao wenyewe. Biashara ya Bajaji ni biashara yenye faida sana, kwa siku mmiliki wa Bajaji anaweza kuingiza kipato cha kati ya Tsh 25,000 mpaka Tsh 30,000 kwa siku, sawa na Tsh 900,000 kwa mwezi, ambayo ni Tsh 10,800,000 kwa mwaka,” alielezea Mpinga.
Bw. Mpinga alisema kwamba kila Bajaji ina thamani ya Tsh 6,700,000. “Tayari Tigo imechukua jukumu la kulipia leseni ya barabara (road license) na bima ya Bajaji. Kwahiyo mteja atakuwa amebakiwa na jukumu la kuja kuchukua Bajaji yake na kuanzisha biashara yake mara moja,” alimalizia Mpinga.