Rais Jakaya Kikwete akisikiliza kwa makini maelezo aliyokuwa akipewa mara baada ya kuingia katika banda la Umoja wa Mataifa Tanzania lililopo kwenye maonyesho ya 37 kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Kikwete akipata maelezo ya kazi mbalimbali zinazofanywa na taasisi mbalimbali za Umoja wa Mataifa nchini.
Ofisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania (UN), Hoyce Temu (kulia), akimkaribisha Rais Jakaya Kikwete kusaini kitabu cha wageni baada ya kumaliza kuzungumza na maofisa wa UN katika banda lao.
Rais Jakaya Kikwete akitia saini kitabu cha wageni katika banda la Umoja wa Mataifa Tanzania. Kulia ni Ofisa Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa Tanzania Hoyce Temu.
Rais Jakaya Kikwete akiangalia moja ya bidhaa za wajasiriamali wanaowezeshwa na Shirika la Kazi Duniani (ILO) wakati alipotembelea banda la Shirika la Umoja wa Mataifa kwenye maonyesho ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar.
Mfanyakazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa nchini akitoa maelezo ya machapisho mbalimbali kwa kijana aliyetembelea banda hilo wakati wa maonyesho ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar.
Ofisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania (UN), Hoyce Temu akifafanua jambo kwa wananchi waliotembelea banda la Umoja wa Mataifa kwenye maonyesho ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea jijini Dar.
Wananchi wakiendelea kumiminika katika banda la Umoja wa Mataifa kupata taarifa mbalimbali za shirika hilo linavyofanya kazi zake na Serikali ya Tanzania.(Picha na http://mwaibale.blogspot.com).