Mratibu wa Tamasha la RAHA ZA JANA NA LEO Bw.Kahabi Ng'wendesha akilitambulisha rasmi Tamasha hilo kwa waandishi wa habari leo jijini Dar katika hoteli ya Chichi iliyopo manispaa ya kinondoni jijini Dar.
Bw. Kahabi alizungumzia namna kampuni ya Yuneda namna ilivyojiandaa kufanikisha tamasha hilo linalosubiriwa kwa hamu na wakazi wa jiji la Dar jumamosi hii katika viwanja vya posta kijitinyama.
Baadhi ya viongozi wa bendi tofauti wakiwa katika mkutano na waandishi wa habari kuthibitisha ni namna gani wamejiandaa naTamasha hilo linalokutanisha bendi sita za muziki wa dansi nchini Tanzania.Bendi hizo ni Mashujaa,Bantu group,Twanga pepeta,Msondo,Sikinde na king kikii"wazee sugu".
Mwanamuziki Bichuka(Sikinde) akifafanua namna watakavyoiburuza Msondo Ngoma jukwaani ikiwa ndiyo waasimu wao wa siku nyingi kwa mara nyingine wanakutana jukwaa moja viwanja vya posta.Pia kutakuwa na silent moment kuwakumbuka wanamuziki wote wa mziki wa dansi waliotangulia mbele ya haki nchini Tanzania.
King Kikii(kushoto) akielezea namna alivyojipanga kuteka mashabiki siku ya jumamosi hii katika viwanja vya posta. Kulia ni mwanamuziki mkongwe Hamza Kalala.Milango ya uwanja itakuwa wazi kuanzia saa tano asubuhi hadi usiku mnene,Watoto bureeee mpaka saa kumi na mbili,wakubwa Tsh 8,000/= tu mpaka chwee.Michezo ya watoto,nyama choma na vinywaji vyakutosha vitakuepo.