Moja ya mambo ambayo ni changamoto kwa manispaa ya Kinondoni ni ujio wa soko hili la Mwenge kituo cha mabasi Madogo jijini Dar es Salaam. Soko hili kila kikicha nalo linakua kwa kasi, kitu cha kujiuliza ni kweli wahusika hawapo? Ama wameamua kuvaa miwani ya mbao? Jambo ambalo limenisikitisha ni wizi unaokuwa unaendelea hapo licha ya vijana kijifanya wamejiajili wenyewe kuuza nguo. Waathirika wakubwa wanaoibiwa ni akina dada kwa maana nguo nyingi zinazouzwa nizao na wao kila unapopita utawakuta wanachagua nguo.
Wito wangu kwa wahusika ni vyema wakafanya mmbadala ili kukinusuru kituo hicho. Kajunason Blog iliweza kufanya mahojiano na mmoja ya wafanyabishara hao na yeye alisema kuwa wao hawana budi kufanya biashara eneo hilo maana linamkusanyiko mwingi wa watu na ndipo maisha yao yanaenda.
'Ndugu mwandishi Usishangae kuona kituo kimejaa meza za biashara eneo hili linalipa sana na wateja wetu wakubwa ni akina dada maana leo hii ukianza kuunza nguo za kiume hapa haupati kitu, wanaume wagumu sana kununua nguo ama vitu ovyo ovyo sehemu kama hizi... Kwa sasa meza moja hapa no sawa na kukodi duka maana ni tunalipia bei ghali sana,' alisema mmoja ya wafanyabisahara hao ambaye hakutaka jinanlake litaje.