Kipindi cha mwanzo cha mahusiano yenu wote mlikuwa na furaha sana, hakuna aliyetamani siku iishe hajamuona mpenzi wake, ofa zote za mitandao ya simu za kulonga bure usiku mlizitendea haki, zawadi nzuri, kadi na maua mlipeana kila wiki, meseji tamu zilizopikwa kwa asali mlitumiana kila sekunde, mliulizana kuhusu kula, kuvaa na mahali alipo mwenzio kila siku, haikutosha hata lile jina alilopewa na wazazi wake ukambatiza na kumpa jingine la sweethert/mpenzi ambalo baba au mama yake hawezi kumuita! sasa umemua mbona vile vyote havipo!!!!?
Ukitaka furaha ya ndoa endeleza vile vya uchumba km huwezi basi ulikuwa unaigiza na movie imefika mwisho! Kama huyo mwenzio hakufanyii hayo muulize mbona siku hizi si kama zamani!?